Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2009


Wasanii wa kundi jipya la TMK UNIT YP(kulia) na Y DASH
Kundi la muziki wa kizazi kipya lililojizolea umaarufu mkubwa kwa mika ya hivi karibuni la Wanaume Family linazidi kumeguka baada ya wanamuziki wake kujiengua na kuanzisha kundi lao jipya la TMK UNIT

Kiongozi wa kundi hilo linaloundwa na watu 3 Jenebi Baraka (Jebby) alisema wamejitoa na sasa wanaandaa albam yenye nyimbo 10 na itaingia sokoni hivi karibuni.

Jebby aliwataja wanamuziki wenzake wanaounda kundi hilo kuwa ni Yesaya Ambikile (YP) na Yassin Habibu(Y DASH) na pia watakuwa na Meneja mpya anayeitwa Issa Abdalah.

Baadhi ya nyimbo zao ni More Fire nyimbo ambayo itatambulisha Albam kufatiwa na Msala Kwao, Siasa Chafu na Himo.

TMK wanaume alimeguka na kutoka TMK Wanaume Halisi iliyokuwa na Juma Nature na TMK Family ya Fella na imejimega tena na kuzaa TMK UNIT.
Posted by MROKI On Friday, January 23, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo