Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2009

Kiongozi wa waasi wa Jamhuri ya Watu wa Kongo, General Laurent Nkunda, amabye aliongoza uasi dhidi ya serikali kwa kiasi kilichozidi ule wa Vita kuu ya pili ya Duania amekamatwa.

Nkunda ametiwa mbaroni usiku wa jana katika nchi jirani ya Rwanda baada ya kupeleka vikosi vitatu vya jeshi kwenda kupambana na vikosi vya pamoja vya Rwanda na Congo alisema Captain Olivier Hamuli msemaji wa kijeshi kwa njia ya simu kutoka mji mkuu wa Goma Kaskazini mwa jimbo la Kivu.

Kukamtwa kwa Nkunda ni mpango uliosukwa kati ya Congo na Rwanda ikiwa ni pamoja na kuyaruhusu majeshi Rwanda kuingia Congo, amesema Jason Stearns, mchambuzi wa kujitegemea wa mambo ya kisiasa.

Kukamtwa kwake kulimkuta wakati akijaribu kuingia nchini Rwanda baada ya kuibuka mapigano na askari wetu katika mji wa Bunagana, Alisema Hamul.

Mji wa Bunanaga upo umbali wa maili 50 au Kilometa 80 kaskazini mwa Goma.

Nkunda alitimuliwa uongozi wa kundi la National Congress for the Defense of the People mapema mwezi huu amesema, wanapigana kulinda utamaduni wa watusti kutoka kwa wanajeshi wahutu ambao walichukuliwa wakimbizi nchini Congo baada ya kushiriki mauaji ya Kimbari ya 1994 nchini Rwanda.

Vita katika ukanda huo emesababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 5 tangu mwaka 1998.
-

Imetafsiriwa kutoka mtandao wa Bloomberg.
Posted by MROKI On Friday, January 23, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo