Nafasi Ya Matangazo

September 29, 2008

Mvua inyeshapo jijini Dar es Salaam huwa ni balaa, pichani ni magari yakiwa yamesongamana katika mitaa ya Samora na Azikiwe katika mzunguko wa Askari jana kufuatia mvua hiyo iliyonyesha kwa saa kadhaa jana. Foleni hii ilidumu kwa zaidi ya saa 7.
Posted by MROKI On Monday, September 29, 2008 3 comments
Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ramadhan 'Chodo' Kikwete (katikati) akiwa na watoto yatima waliofika Ikulu Dar es Salaam kwaajili ya kufuturu. Rais kupitia kwa Mnikulu alifuturisha watoto yatima kutoka katika vituo mbalimbali vya Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Monday, September 29, 2008 3 comments

September 28, 2008

Mkazi wa Kigogo mwisho Dar es Salaam akichota maji kwenye bomba la maji lililopasuka katikati ya mreji wa maji taka unaopita eneo hilo jana. Uchotaji maji wa namna hii ni hatari maana amiminapo maji hayo katika ndoo nyingine hudondokewa na matone ya maji taka.
Posted by MROKI On Sunday, September 28, 2008 1 comment
Mhariri wa Picha wa Magazezeti ya HabariLeo na HabariLeo Jumapili, Athumani Hamisi akipandishwa katika gari la wagojwa tayari kwa safarai ya uwanja wa ndege ambako alikuwa akisafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi kufuatia ajali ya gari aliyoipata mamepa mwezi huu Wilayani Kilwa. Athumani aliumia zaidi kifua na shingo alisafirishwa jana kwa ndege ya ATCL.
Blog hii inamuombea kwa Mungu amjalie afya njema haraka na matibabu mema.
Posted by MROKI On Sunday, September 28, 2008 1 comment

September 25, 2008

Mkazi wa jiji la Dar es Salaam (kushoto) akimwangalia mtu mwenyeulemavu aliyekuwa akishuka ngazi za kuingilia katika ofisi za Mahakama ya Kazi zilizopo katika jingo la NSSF jijini Dar es Salaam jana. Usumbufu kama huu unawapata walemavu wengi wanaotembelea majengo mengi nchini ambayo hayana njia maalum za kuingilia walemavu ni vyema mamlaka husika na wakandarasi wakazingatia mahitaji ya watu wenyeulemavu katika ujenzi.
Posted by MROKI On Thursday, September 25, 2008 No comments

September 24, 2008

Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi Lawrence Masha (kushoto) akipanda moja ya pikipiki zilizotolewa na Kampuni ya BlueFinancil ya Jijini Dar es Salaam kwa Polisi, Katikati ni Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Synarge Navin Kanabar na kulia ni Mkuu wa Polisi Tanzania (IGP) Saidi Mwema. Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salalaam.
Posted by MROKI On Wednesday, September 24, 2008 No comments
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga akipita mbele ya gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere Dar es Salaam jana. Kulia kwa Odinga ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Abdalah Kihato.
Posted by MROKI On Wednesday, September 24, 2008 No comments

September 23, 2008





Vimwana toka Mohagany Models nchini Uingereza wajkionyesha mavazi yaliyobuniwa an Ally Remtula wakati wa maonyesho ya mavazi yaliyofanyika katika jumba la Makumbusho nchini Ungereza.
Posted by MROKI On Tuesday, September 23, 2008 No comments
Jidada amerejea leo toka jumba la BBA III
Posted by MROKI On Tuesday, September 23, 2008 No comments
TAARIFA AMBAZO ZIMEIFIKIA BLOG HII HIVI PUNDE ZINASEMA MWANDISHI WA MAGAZETI YA UHURU NA MZALENDO RAMADHANI KINYONYA ALIYEKUWA AMELAZWA KWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI AMEFARIKI DUNIA.
BLOG HII INAWAPA POLE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NA WANAHABARI WOTE KWA UJUMLA KUTOKANA NA MSIBA HUU MZITO.

MUNGU ALAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA AMINA.
Posted by MROKI On Tuesday, September 23, 2008 No comments
HUDUMA ZA MLIO KWA MPIGAJI SASA BEI CHEE

Mburudishe akupigiae kwa shilingi 27 tu kwa siku (Caller Tune Services)

Sasa Tigo imepunguza gharama za Mlio kwa Mpigagaji (Caller Tune) Hii ni huduma inayomruhusu mteja kuweka wimbo kwenye simu yake ili ampigiae aweze kuusikia midundo miziki kabambe badala ya mpigaji kusikia mlio wa "ring ring".

Namna ya kupata huduma hii.

1) Mteja anapaswa kupiga namba 15007 na kufuatisha maelekezo atakayopewa.

Punde atapata wimbo anaoutaka anatakiwa kufuata maelekjezo ya nini cha kufanya hapohapo ili kunakili wimbo huo kwenye simu yake.

Gharama ya (Caller Tune services) mlio kwa mpigaji ni shilingi 27 tu kwa siku.

TIGO EXPPRESS YOURSELF.
Posted by MROKI On Tuesday, September 23, 2008 No comments

September 22, 2008

Mmoja wa maafisa walioko kwenye msafara wa Waziri Mkuu, Bw. Hamisi Kamundu akijaribu kupiga simu kwenye eneo pekee ambalo mtandao wa Vodacom unapatikana katika kijiji cha Mapili wilayani Mpanda kama maandishi ya nyuma yake yanavyoonyesha.
NB: Makampuni ya simu vi[pi mnasema mnasema mpo nchi nzima?
Asante Kamanda Irine Bwire kwa snape hii.
Posted by MROKI On Monday, September 22, 2008 No comments

September 20, 2008

Nilifanyiwa mshtuko kidogo juu ya keki hii na my wife.

Wadau keki hii sijaila nawasubiri hivyo kila atakae katika maskani atapata kipande maana ni kubwa na haaiishi leo wala kesho, iwapo kama mimi sipo basi unisubiri walae upate kipande. Niliadhimisha mika kamili ya kijana namshukuru mungu ujana wangu umeingia nikiwa na watoto wawili. Pia Septemba 18 ilikuwa ni mwaka mmoja tangu kufariki kwa baba yangu Mzee S T Nathan.

Posted by MROKI On Saturday, September 20, 2008 3 comments
Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia (fFU) akifyatua bomu la machozi kuwasambaratisha mashabiki wa timu ya Simba waliokuwa wanataka kuwashambulia waamuzi wa mchezo katika ya Simba na Polisi Dodoma katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka uwanjani 2-2 na kuifanya Simba kushindwa kufurukuta kwa timu zote za Majeshi kwani Ilishafungwa na Prisons 1-0, JK Ruvu 1-0 na sasa Polisi 2-2.
Posted by MROKI On Saturday, September 20, 2008 No comments





Baadhi ya wafanyakazi 8 wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) waliofikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu jijini Dar es Salaam jana kujibu tuhuma za kughushi vyeti wakijifunika nyuso zao kuwakwepa paparazi Septemba 20 wakati wakienda kupanda karandinga tayari kwa safari ya Mahabusu hadi Oktoba 6 shitaka lao litakapo anza kusikilizwa.
Wafanyakazi hao, ni Justina J Mungai, ambaye imeelezwa kuwa ni mtoto wa Joseph Mungai, ambaye amewahi kushika wizara tofauti ikiwemo ya elimu, Christina G Ntemi, Siamini Eddie Kombakono, Janeth John Mahenge, Beatha Constantine Massawe, Jacquiline David Juma, Philimina Philibert Mutagurwa na Amina Mohamed Mwinchumu.
Posted by MROKI On Saturday, September 20, 2008 No comments

September 18, 2008

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la HabariLeo Athumani Hamisi aliyepata ajali wiki iliyopita. Serikali imeahidi kushughulikia matibabu yake haraka nje ya nchi.

Baba mzazi wa Athumani, Mzee Hamisi Msengi akifariji mtoto wake Hospitalini hapo jana.
Posted by MROKI On Thursday, September 18, 2008 No comments

September 17, 2008

Zephania Musendo akilakiwa na kupewa kumbato kutoka kwa mkewe kipenzi Pascalia mara baada ya kuonana kwa mara ya kwanza nje ya gereza la Mahabusu Mkuza mkoani Mpwani.
Mwandishi Mwandamizi Zephania Musendo akionyesha ishara ya kuwa huru baada ya kumaliza kifungo chake.
Msendo atoka kifungoni akiwa na furaha.
*aiteua siku ya kutoka jela kuwa ya kuzaliwa
*aha hidi kuendelea kuandika maovu
*
Na Mroki Mroki Kibaha
MWANDISHI wa Habari Mwandamizi, Zephania Musendo aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano jela ametoka gerezaji jana.

Musendo aliyeanza kutumikia kifungo chake Mei 17, mwaka 2005 katika gereza la Keko kwa kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa aliachiwa saa 9:54 na kupokelewa na wanafamilia yake waliofika kumpokea katika gereza la Mahabusu Mkuza mkoani Pwani.

Musendo aliyelakiwa na watoto wake Richard na Victor, mke wake Pascalia pamoja na shemeji yake Elizabeth N’gabo aliiteua siku yake ya kutoka gerezani na kuwa siku yake ya kuzaliwa baada ya yeye kutokuifahamu rasmi tarehe yake ya kuzaliwa.

“Leo ni siku yangu ya kuzaliwa maana ninafurahi sana kuwa hutru na kutoka katika matatizo haya ambayo yamenikabili kwa kipindi kirefu, baba yangu hakujua nilizaliwa lini zaidi ya mwaka kuwa ni 1947,”

Wanafafamilia hao wanasema wanafurahi sana babayao kuwa huru na wanamshukuru Mungu kwa kutoka jela akiwa hai na mwenye afya njema tofauti na walivyodhania.

Akisimulia maisha yake ya miaka mitatu na miezi mitano aliyoishi katika magereza mawili ya Keko na Mkuza anasema ni maisha hatari yasiyozoeleka na mwanadamu wa kawaida.

“Jela hakufai maana kitendo cha kutengwa na jamii, familia yako, nyumba ndugu jamaa na marafiki na kufanya mambo yako kwa uhutru ni hatari sana,” alisema.

Anasema alipokaa katika gereza la Keko kwa muda wa mwezi mmoja mambo hayakuwa mazuri sana kutokana na afya yake kutokuwa nzuri nay eye kulazimika kutumikia kifungo sambamba na kazi ngumu.

Licha ya kuwa hakupata usumbufu wa mateso kutoka kwa wafungwa wenzakwe lakini alipata tabu mwanzoni kutoka kwa Askari Magereza kwa kutekeleza adhabu yake kwa upande wa kazi ngumu.

“Nilipata shida kutoka kwa askari maana walikuwa hawanielewi kuwa ninaumwa , wao walishikilia midhali nimehukumiwa kazi ngumu lazima nizifanye tu,” alisema.

Alisema wakati akiwa katika gereza la Mkuza mkoani Pwani wakifabnya kazi ya kubeba kifusi katika jingo la Mkuu wa Mkoa alianguka katika ngazi na kushindwa kuendelea na kazi lakini hakupelekwa Hospitali siku hiyo kupatiwa matibabu.

Alianza kupatiwa matibabu ya Kisukari pamoja na Presha katika Hospitali ya Tumbi na kuandikiwa na daktari awe anakula mayai, maziwa na mboga za majani lakini aliporudi gerezani hakupata vitu hivyo hadi pale familia yake ilipoamua kumuwekea bili ya maziwa kutoka katika Ng’ombe gerezani hapo.

Aliendelea na kazi nyepesi gerezani hadi pale alipochaguliwa kuwa Nyapara mkuu Aprili 2007 nafasi ambayo aliitumikia hadi alipotoka gerezani humo.

Baadhi ya Askari Jela walisema watamkumbuka Musendo kwa nidhamu, Busara na Uongozi mzuri alipokuwa Nyapara mkuu katika gereza hilo ambalo linawafungwa 78 na mahabusu 129.

Aidha Musendo anasema maisha yake yalibadilika pale alipochaguliwa kuwa Nyapara mkuu na wenzake kumkubali na kumheshimu kutokana na umri wake.

“Kazi zangu kubwa zilikuwa kusimamia chakula, magenge ya kazi, usafi wa gereza na uandaaji wa risala kwa wageni zihusuzo wafungwa… kuna wakati niliandika hata risala za mkuu wa Gereza”.

Akizungumzia juu ya tuhuma zilizo mtia hatiani Musendo anasema yeye kwa sasa anafurahi na kushukuru Mungu kuwa yupo huru lakini Kubwa zaidi anafurahia kuwa habarizilizokuwa zikiandikwa katika gazeti zilikuwa ni zakweli.

Juu ya kurejea katiika ulingo wa habari Musendo anasema hatoacha kuandika na kampuni yeyote atakayopata ataanza kazi yake ya uandishi na kulitumikia taifa.
NB:
Gazeti la HabariLeo ndio gazeti pekee lililopata picha za tukio hili pamoja na Habari. Usikose Makala yake toleo la Septemba 18 2008 katika HabariLeo. www.habarileo.co.tz
Posted by MROKI On Wednesday, September 17, 2008 No comments

September 14, 2008

Walimu wa shule 18 za Wilaya ya Kilolo wakipiga picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla (wa tano kushoto nyuma) baada ya kukabidhiwa vitabu wilayani Kilolo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe. Zain ilitoa vitabu vyenye thamani ya sh. milioni 18.
Posted by MROKI On Sunday, September 14, 2008 No comments
Habari ya kazi kaka zangu wapenzi, I hope tunaenda sawa na mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mimi ni mjasirimali mwenzenu na sasa nimepania kuwakwamua wenzangu kiuchumi. Nimeandaa semina kubwa Millenium Tower 'Makumbusho' Semina hiyo inahusu jinsi ya kujikwamua kiuchumi na mtu kutoka katika umaskini. Lengo letu ni kusaidiana ili kujiinua, Mtaji tunao ni sisi wenyewe kuchukua hatua. Semina hiyo itakua J.5 saa 8 mchana na J.mosi saa 8 machana. Kutokana na blog yako kutembelewa na watu wengi wa rika mbali mbali naomba uniwekee katangazo kaka hata na wewe unakaribishwa. Hakuna kiingilio ni bureeeee....
Kwa watakaofika wasiliana na no. 0767 17 77 74
Posted by MROKI On Sunday, September 14, 2008 1 comment

September 12, 2008

Gari ambalo alikuwa akisafiria Athumani Hamisi, Hery Makange na Anthony Siame T 961 AGT baada ya kupata ajali.
Herry Makange akimsaidia Athumani mara baada ya kumtoa katika gari Baadhi ya wananchi waliofika katika tukio hilo. Inasikitisha majeruhi waliibiwa baadhi ya vitu vyao vikiwamo fedha na simu za mkononi.
Posted by MROKI On Friday, September 12, 2008 1 comment
Athumani Hamisi akihamishwa wodi jioni 12-9-08. Athumani aliyepata ajali asubuhi leo amelazwa katika wodi ya Sewahaji 17 wakati mipango ya kumhamishia katika wodi Maalum inafanyika. Blog hii inampa pole sana Athuman na kumuombea heri apone haraka.
Posted by MROKI On Friday, September 12, 2008 1 comment
Mabalozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain Judith Wambura (kulia) na Issa Muhidin Michuzi wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Zain, Costantine Magavilla (katikati) wakati wa kuwatangaza mabalozi hao jana.
Posted by MROKI On Friday, September 12, 2008 No comments
Herry Makange (kushoto) na Athuman Hamisi.

Wapigapicha za Habari wa tatu wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo wamenusurika kufa katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi wakiwa njiani kelekea Kilwa katika futari maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Vodacom kupitia Voda Foundations. Wapigapicha hao ni Athumani Hamisi wa Daily News na Habarileo, Herry Makange wa DTV na Channel 10 pamoja na Anthony Siame wa New Habari Cooparation. Halizao zinaendelea vyema isipokuwa Athumani aliyepata majeraha kichwani tumboni na mkononi baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka mara tatu. Athumani kwa sasa yupo Hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu na yupo wodi ya Dharula.
Posted by MROKI On Friday, September 12, 2008 No comments

September 05, 2008


Rais wa Chama Tawala Afrika Kusini (ANC) Jacob Zuma (kulia) akisikilizwa maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Profesa Gerald Monela kuhusu picha za wapigania Uhuru wa Afrika Kusini waliokuwa wakiongozwa na Lilian Ngoyi zilizochorwa katika moja ya kuta za Chuo hicho Mazimbu mkoani Morogoro juzi.
Posted by MROKI On Friday, September 05, 2008 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo