Nafasi Ya Matangazo

May 26, 2024





Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amesimamia ubomoaji wa karavati moja kati ya sita, lililokuwa linaendelea kujengwa,  katika mradi wa shilingi 111,822,000 (Mil. 111) wa barabara ya l
kilomita 5  wa Lyabusalu Mwajiji - Halmashauri ya Shinyanga Vijijini.  

DC Mtatiro akiambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Shinyanga, amefika katika moja ya makaravati ya mradi huo na kukuta ujenzi ukiendelea huku uwiano wa simenti na mchanga ukionesha simenti imechakachuliwa.

DC Mtatiro amemtaka Meneja wa TARURA Wilaya ya Shinyanga aeleze ikiwa anaridhishwa na hali hiyo, Meneja huyo mbele ya Kamati ya Usalama amekiri ni kweli simenti imechakachuliwa na kwamba mkandarasi amejaza mchanga zaidi kuliko simenti na kwa hiyo hakuna uwiano. Meneja amejitetea kuwa kwa bahati mbaya Afisa wa TARURA aliyempanga kusimamia mradi huo alikuwa ametoka kidogo ndipo mkandarasi akachakachua simenti.

DC Mtatiro akiwa eneo la mradi amemuhoji mkandarasi wa kampuni ya M/S AM & PARTNER LIMITED ya jijini Dar Es Salaam, ambayo inatekeleza mradi huo, ambapo mkandarasi amekiri kuna upungufu.

Katika hatua nyingine Wakili Mtatiro ameelekeza makaravati yote yaliyotengenezwa kwenye mradi huo yahakikiwe kwa vipimo maalum vya madaraja, kabla ya kuchukua hatua kali zaidi ikiwemo kum-blacklist mkandarasi husika wilayani Shinyanga.

Wakili Mtatiro amemuonya Meneja wa TARURA Wilaya ya Shinyanga na kumtaka atekeleze majukumu yake ipasavyo na amepanga kikao maalum na Wakandarasi wote ili kutoa maelekezo ya kiserikali ya utekelezaji wa miradi kwa ubora.
Posted by MROKI On Sunday, May 26, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo