Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2024





Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wachezaji wa timu ya Mahakama Tanzania wamechanua katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), kwa kufanya vema kwenye mbio za mita 800 na 3000 kwa upande wa wanawake zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Mchezaji Yusta Tibendeka wa Mahakama ndio aliyeshinda mita 800 kwa kutumia muda wa dakika 2:48.47 na baadaye katika mbio za mita 3000 kwa muda wa dakika 12:13.62.
Yusta alifuatiwa na Martha Kunzugala wa TAKUKURU katika mbio za mita 800 aliyetumia muda wa dakika 2:53.5 ambaye pia alishika nafasi kama hiyo kwenye mita 3000 kwa muda wa dakika 12:34.75; na mshindi wa tatu katika mbio hizo mbili (800 na 3000)  ni Nyamiza Ndibalema wa Wizara ya Madini aliyetumia muda wa dakika 3:00.9. na  na dakika 12:58.01.

Katika mbio za mita 3000 kwa wanaume ubingwa umechukuliwa na Paulo Remmy wa Ofisi ya Rais Ikulu aliyetumia muda wa dakika 9:16.90, wakati ushindi wa pili umekwenda kwa Aidan Adrean wa Wizara ya Uchukuzi aliyetumia dakika 9:38.89 na mshindi wa tatu ni Joseph Kachala wa Wizara ya Afya aliyetumia muda wa dakika 9:51.06

Katika mchezo wa kurusha tufe kwa wanawake Theodora Sallema wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ametwaa ubingwa kwa kurusha umbali wa futi 9:42;  akifuatiwa na Emid Geofrey wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora aliyerusha futi 8:05 na watatu ni Liliani Mwabulanga wa Wizara ya Elimu na Teknolojia ya Ufundi alirusha futi 8:02.

Kwa upande wa wanaume bingwa ni Sifael Msenga wa RAS Tanga kwa futi 9:49; akifuatiwa na Onesmo Lubeleje wa Wizara ya Elimu kwa futi 9:13 na wa tatu ni Jackson Venance wa Wakala ya Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa futi  9:10. 
Katika mbio za watu wazima kuanzia umri wa miaka 50 kwa wanawake ubingwa umechukuliwa na Abelina Stephano wa Msajili wa Hazina, akifuatiwa na Monica Katema wa Ofisi ya Bunge na watatu ni Fatma Seif wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
 
Michezo ya riadha itaendelea tena Septemba 30, 2024 katika hatua ya nusu fainali na fainali kwa mbio za mita 800 (wanaume), 100, 200, 400 (wanawake na wanaume), pia mbio za watu wazima mita 100 (wanaume), mitq 1500 na kupokezana vijiti 4x100, ambao tayari wameshacheza hatua ya awali na kufuzu hatua hiyo.

Halikadhalika michuano hii ya SHIMIWI kesho tarehe 27 Septemba, 2024 inaingia katika hatua ya 16 bora kwa michezo ya kuvutana kwa kamba, mpira wa netiboli na miguu.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo