Nafasi Ya Matangazo

November 09, 2017

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, ameagiza Viongozi wote waliohusika kupokea mifugo Pamoja na wafugaji kutoka Nje ya nchi kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Mpina amesema pindi uchunguzi ukikamilika miongoni mwa hatua zitakao chukuliwa ni pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji watakao gundulika walijihusisha na suala hiloni kinyume na maadili ya utumishi wa uuma.

Hata hivyo waziri huyo aliongoza zoezi la ukamataji wa Ng'ombe zilizo ingizwa nchini kinyume na utaratibu jumla ya Ng'ombe 1580 wanashikiliwa na  kuagiza Ng'ombe hizo zitaifishwe  na kupigwa mnada baada ya uchunguzi kukamilika na kuhakikisha ifikapo Novemba 10 mwaka huu Mifugo yote iliyoingia kinyume na utaratibu ziwe zimeondolewa kabisa.

Akizungumza juzi mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Mpina alisema   viongozi walioshiriki kupokea mifugo kutoka Nje ya Nchi washughulikiwe kisheria kwani hawawezi kuwa na viongozi wanowahifadhi wahalifu wanaoingia Nchini bila kujali masilahi ya nchi.

Alisema mifugo hiyo imekuwa kero kwa kuharibu Mashamba ya wananchi na Katika maeneo mengi ya hifadhi yameharibiwa na Wavamizi hao.

Zaidi ya mifugo 9,500 imekamatwa chi anima na itatakiwa kutaifishwa baada ya wanasheria na maafisa uhamiaji kuthibitisha kuwa iliingia kinyume cha sheria ilikuifanyia mnada na kukomesha wavamizi wote wanaoingia kinyume na utaratibu na kuharibu misitu na kuwa kichocheo cha migogoro ya wakulima na Wafugaji katika Maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu  ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marco Gaguti alisema katika msako walioufanya wilayani humo wamefanikiwa kukamata Ng'ombe 1,580 na kwamba mpaka sasa wanaendelea na oparesheni ya kusaka mifugo hiyo ilikuhakikisha ifikapo Novemba 10 mifugo hiyo iweimekwisha ondoka  na kuhakikisha hakuna mifugo mingine inayoendelea kuingia kinyume na utaratibu.

Aidha Mkuu  huyo alisema ,wapo baadhi ya viongozi walioshirikiana na wafugaji kwa kupokea fedha na kuruhusu mifugo hiyo iendelee kuishi Nchini bila utaratibu, uchunguzi  unaendelea kuwabaini na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakao bainika huku akisema upelelezi unaendelea kufanyika kwa  haraka kuhakikisha kuwa wamesafisha maeneo yote ambayo yamevamiwa na Wafugaji kutoka Nje na kuwabaini wale wote walioshirikiana nao.

Hata hivyo aliwaomba  Wananchi kuendelea  kutoa taarifa endapo kunawafugaji waliingia katika maeneo yao bila utaratibu na kuacha kuwahifadhi ilikuepusha migogoro ya Wafugaji na wakulima kutokana na wafugaji hao kuingilia maeneo ya wakulima.
Posted by MROKI On Thursday, November 09, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo