Nafasi Ya Matangazo

September 19, 2024


Na Mwandishi wetu, Zanzibar 
Imeelezwa kwamba mpango mzuri wa ufuatiliaji na tathimini umewezesha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufikia malengo ambayo wamejiwekea katika kutekeleza dhima ya taasisi hiyo ya kujenga na kufanya matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya nchini.

Akiongea kwenye Kongamano la Tatu la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji,Tathimini na mafunzo yanayoendelea kwenye hotel  ya Golden Tulip, Zanzibar, Meneja Mipango wa TARURA Bw. Justin Lyatuu amesema kwamba namna ya kujua wamefikia lengo walilolipanga kwenye dira yao lazima wahusishe ufuatiliaji na tathimini.

“Kupitia ufuatiliaji ndipo tunafanya tathimini ili kuona kwanini hatufikii hatua na kama kuna kikwazo basi tunarudi nyuma kuangalia tatizo ni nini na hivyo tunaendelea kupima ili jamii iendelee kupata huduma za kijamii kwa kutumia barabara”.

Amesema Kongamano hilo linawaongezea uelewa kwani wao kama TARURA kwa matengenezo ya barabara lengo lao ni kuwaunganisha wananchi  kwa kupita kwenye barabara nzuri.

Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambalo wametembelea banda la TARURA wamepongeza Wakala kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufungua barabara za wilaya na hivyo kuwasaidia wananchi kuinuka kiuchumi kwakuwa hivi sasa wanaweza kusafirisha mazao yao kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Posted by MROKI On Thursday, September 19, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo