Nafasi Ya Matangazo

March 03, 2017

 Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akipokewa kwa furaha na mmoja wa watoto wake alipowasili nyumbani kwake hii leo akitoka mahabusu.
 Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alipowasili nyumbani kwake hii leo.
Bety Alex, Arusha
Mahakama kuu kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema.

Lema ameachiwa  kwa dhamana ya sh milioni moja pamoja na wadhamini wawili  wenye vitambulisho vinavyotambulika na serikali.

Akisoma hukumu ya Mbunge Lema katika Mahakama Kuu Arusha Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Salma Magimbi amesema kuwa Mbunge  Lema hakupaswa kukaa  mahabusu mda mrefu kwani ilipaswa kupewa dhamana.

Jaji magimbi amesema kuwa wanamwachia lema kwa dhamana hiyo ya milioni moja ambapo kiasi hicho  kimetolewa kwa njia ya bondi huku wadhamini wawili nao wakiwa na vigezo vya dhamana.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo Mbunge Lema amesema kuwa Jamhuri ilikuwa na nia ya kumfunga lakini mungu amempigania mpaka kutoka huku akimshukuru mke wake kwa jinsi alivyomfariji kwa kipindi akiwa ndani.

Alisema kuwa kwa sasa ameandaa waraka wa kumwandikia raisi kuwa wapo watu wanaoteseka bila kuwa na hatia magereza na kwamba atautoa hivi karibuni

Nae wakili mtetezi wa Lema, Peter Kibatala alisema kuwa Mahakama kuu imelekeza kuwa mahakama za chini zisimamie madaraka yake na mamlaka yake bila kuyaachia na hivyo kwa sasa wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya kupambana na kesi.

Nae Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe alisema kuwa wanamkaribisha tena Lema Bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza vikao vyake mjini hapa na kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali waliofika kutetea dhamana ya lema.

Aidha Mbowe amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwapiga wananchi bila makosa kwa madai kuwa wanakuja kuleta vurugu huku lengo ni kuja kusikiliza mbunge wao.
Posted by MROKI On Friday, March 03, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo