Nafasi Ya Matangazo

March 16, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala akifyeka shamba la bangi iliyokamatwa katika msako maalum wa dawa za kulevya Wilayani humo ambapo zaidi ya heka tatu zilikutwa zimelimwa katika hifadhi ya akiba ya  wanyama pori ya Kigosi Moyowosi
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (mwenye kombati) akisaidia kupanga kuni kwaajili ya kutekeza bangi iliyokamatwa katika msako maalu wa dawa za kulevya mkoani Wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko akitumia bodaboda kwenda katika msako wa bangi.
  Mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika msako huo akilima bangi akiwa chini ya ulinzi. 
************
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
JUMLA ya hekari nne za mashamba ya bhangi zimeteketezwa  kwa moto Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma pamojoa na watuhumiwa watatu waliokuwa wakijihusisha na ulimaji wa  zao hilo haramu kutiwa mbaroni .

Uteketezaji huo umefanyika katika msako maalum ulioanza mapema wiki hii ukihusisha Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kakonko.

Akiongoza zoezi la uteketetezaji wa bhangi hekari tatu zilizo kutwa zimelimwa katika hifadhi ya akiba ya  wanyama pori ya Kigosi Moyowosi Wilayani humo  jana,  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alisema kamati ya ulinzi na usalama ilipata taarifa kutoka kwa Wananchi wanaochukia uhalifu kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo kunawatu wanalima bhagi ndipo walipo amua kuanza msako huo.

Kanali Ndagala alisema zoezi hilo la kuwasaka walima bhangi na kuteketeza bhangi iliyo kutwa katika mashamba ya walima bhangi, limeanza jumatatu ya wiki hii na mpaka sasa wamefanikiwa kuchoma hekari nne za mashamba ya bhangi na kukamata watuhumiwa watatu waliokuwa wakijihusisha na ulimaji wa zao hilo ambapo shamba moja walitembea mwendo wa masaa manne kwa piki piki hadi kufikia eneo hilo wanalo lima .

Alisema katika hifadhi ya akiba ya Wanyama pori walifanikiwa kukamata shamba lenye hekari tatu na mtuhumiwa, Ntibalima Masuhuko Mkazi wa Kazuramihunda aliekutwa katika shamba hilo na  Kijiji cha Mbizi kitongoji cha Nyangereke waliteketeza shamba la bhangi hekari moja na kukamata watuhumiwa wawili waliokuwa wakilima shamba hilo.

Hata hivyo Kanali Ndagala alisema zoezi hilo ni endelevu wataendelea kuwasaka wote wanao lima bhangi kokote pale walipo hata majumbani kwao ilikuhakikisha wanaokoa Vijana walio asilika na dawa za kulevya ambao wengi wao wanadhiriki hata katika vitendo vya wizi na ujambazi kutokana na msukumo wa dawa hizo.

"Nitoe onyo kwa Wafanya biashara wa dawa za kulevya waache tabia hiyo serikali yetu inamacho kila kona na watoto wengi wameharibikiwa kwasababu ya tamaa za watu wachache kupata utajiri wa haraka  kwa yeyote tutakae mbaini tutamchukulia sheria ilikuwa fundisho kwa wengine , nimeona kwa sasa tumejitahidi kuzuia uuzaji wa bhangi kwassa haipatikani sana mitaani tuta hakikisha haipo kabisa", alisema Mkuu huyo.5

Kwa upande wake Mtuhumiwa mmoja aliekutwa katika Shamba la bhangi hekari tatu huko hifadhini ,Ntibalima Masuhuko alidai kuwa alikabidhiwa shamba hilo awe kama mlinzi na kudai mimea hiyo ya bhangi kwamba ni Magugu tuu yaliyo kiwa shambani na hana uelewa wowote kuhusiana na mmea wa bhangi.
Posted by MROKI On Thursday, March 16, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo