Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro (katikati), akizungumza kwenye semina elekezi kuhusu uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa wananchi, iliyofanyika Jijini Mwanza leo.
Washirki wa semina hiyo
Wanasemina. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Wanasemina
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina akihojiwa na wanahabari
Picha ya pamoja
******************
Na BMG
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, imewahimiza wananchi kuzingatia matumizi sahihi na
endelevu ya kondomu ili kujiepusha na mimba zisizotarajiwa pamoja na magongwa
ya kuambukiza ikiwemo virusi vya Ukimwi.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari,
elimu na mawasiliano kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah
Katikiro, ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza, kwenye semina elekezi kuhusu
uzinduzi wa Kondom mpya ya Zana itakayokuwa ikitolewa bure na serikali kwa
wananchi.
Katikiro amesisitiza matumizi sahihi
na endelevu ya kondom ya Zana kwa wananchi walio kwenye mahusiano ya kimapenzi,
yatasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama virusi vya Ukimwi
pamoja na mimba zisizotarajiwa na kwamba aina hiyo ya kondom ni imara na yenye
ubora.
Mratibu wa mpango wa Taifa wa
kudhibiti Ukimwi, mkoani Mwanza, Geofrey Mabu, amesema mkoa wa Mwanza
umejipanga vyema ili kuhakikisha kondom za Zana zinawafikiwa walengwa hususani
kupatikana bure katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye vituo vyote vya afya,
maeneo ya starehe pamoja na kwenye ofisi za serikali na binafsi.
Uzinduzi wa Zana Kondom kitaifa
ulifanyika mkoani Mbeya wiki iliyopita ambapo kwa mkoa wa Mwanza uzinduzi
utafanyika kesho Jijini Mwanza ambapo aina hiyo ya kondomu itakuwa mbadala wa
kondom za MSD zilizokuwa zikitolewa pia bure na Serikali lengo likiwa ni
kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa.Bonyeza HAPA Kujua Zaidi
0 comments:
Post a Comment