Nafasi Ya Matangazo

February 04, 2016

Katibu wa Jumuia na Taasisi za kiislam Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kutoa msimamo wa Jumuia ya Kiisalam,u na Taasisi zake kuhusiana na suala la uchaguzi wa Zanzibar na kumuomba Rais John Magufuli kuingilia kati suala hilo.
*********************
KWA mara ya kwanza tangu atoke mahabusu, Katibu wa Jumuia na Taasisi za kiislam Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda amezungumza na vyombo vya habari na kukanusha taarifa ya za kiongozi wa Uamsho kuunga mkono uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar.

 Juzi akizungumza na vyombo vya habari, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, alisema amepokea barua kutoka kwa Amir wa Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmad ambaye yuko gerezani, akieleza kuunga mkono suala la kufanya uchaguzi wa marudio kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro huo, na kuwa hakuna njia mbadala.

 Shehe Ponda alisema kuwa Shehe Farid amewatuma kukamnusha madai hayo na kuwa yeye hajamtuma mtu yeyote kuzungumzia suala hilo.

 “Tumemtembelea Shehe Farid gerezani, lakini pia tulikutana na wanasheria wake pamoja na viongozi wa gereza kutaka kujua kama aliandika barua yeyeyote na si yeye wala mwanasheria au magereza waliothibitisha kufanya hivyo nae kutuomba kukanusha taarifa hizo na kusema hazina ukweli wowote,” alisema Shehe Ponda.

Ponda amemtaka Rais John Magufuli kutekeleza ahadi yake aliyoitoa Bungeni juu ya kufuatilia hatma ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na kutoa tamko la yale yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kutafuta suluhu yaliyokuwa yakihusisha pande mbili zinazo vutana za Chama cha Wananchi CUF na Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Rais achukue ahadi yake aliyoitoa Bungeni, anawajibu wa kuitekeleza kwa vitendo na ahakikishe mzozo huu anaupatia ufunbuzi bila ya kuitumbukiza Zanzibar kwenye dhiki na  uhasama,” alisema Ponda.  SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Pia alisema kuwa vyombo vya usalama vilivyopo Zanzibar vipo kwa amri yake hivyo ebndapo patatokea jambo lolote kabla ya kumaliza mzozo wa kiauisa uliopo visiwani humo ni yeye atakae laumiwa.

Aidha akizungumzia kuhusu uchaguzi Mkuu wa Zanzibar iliofanyika Oktoba 25 mwaka jana nchini kote ukisimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Ule wa Zanzibar uliosimamiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kasha ZEC kufuta matokea yake na kutangaza kurudiwa tena Machi 20 mwaka huu, kuwa uchaguzi huo ulikuwa mzuri na halali huku  NEC na ZEC zikifanya kazi yao vizuri.

“Uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 kwa pande zote za Muungano uliosimamiwa na NEC na ZEC ulikuwa halali na mchakato wake kwa ujumla ulikwenda vizuri  kwani Rais  wa Muungano Wabunge, Madiwani, wawakilishi  wamepatikana kwa uchaguzi huo, Sehemu ya Zanizbar Wabunge wa Bunge la Muungano pia wamepatikana kwa uchaguzi uliosimamiwa na ZEC na matokeo yake tunayaheshimu,”alisema Shehe Ponda.
Ponda alisema kuwa wao kama Jumuia na Taasisi za kiislam  wanaungaa mkono hatua za mwanzo zilizochukuliwa kunusuru hali ya kisiasa Zanzibar kwa kufanya mazungumzo baina ya vyama hasimu vya CUF na CCM pamoja na kuunga mkono ahadi ya Rais John Magufuli ya kushughulikia mzozo huo aliyoitoa Bungeni.

Amehoji ukimya uliopo hadi sasa kwani watanzania hawajapewa taarifa ya pamoja kutoka CCM na CUF kuhusiana na mazungumzo waliyofanya yameishia wapi na yapi wamekubaliana na yapi hawajakubaliana na nini hatima ya mazungumzo yao.

Ponda alisema kuwa Jumuia na Taasisi za kiislam inapinga vikali uamuzi wa ZEC kutangaza tarehe ya kurudia uchaguzi kabla ya ufumbuzi wa mambo ya msingi na ya kisheria kupatikana kwani hatua hiyo inaweza kuleta fujo na uhasama na kuharibu utangamano uliopatikana kwa kipindi cha miaka ya karibuni Zanzibar.

Katika hatua nyingine Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Rajabu Katimba amesema kuwa vyama vya siasa, Msajili wa vyama vya siasa na wananchi wote wakemee na CCM ifute kauli na kuwaadhibu wanachama wake waliotoa kauli za kuwa CCM Zanzibar ahitatoa serikali kupitia sanduku la kura (karatasi) kwani ni nchi ya Mapinduzi na pia kauli za kibaguzi ilizotolewa kwa njia ya mabango hivi karibuni.
Posted by MROKI On Thursday, February 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo