Nafasi Ya Matangazo

July 13, 2015

IGP, Ernest Mangu 
WATU walio na silaha za moto wamekivamia kituo cha Polisi Staki Shari Ukonga na kuwaua watu 7 wakiwepo Polisi wanne.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa askari waliouwawa ni wanne na rais watatu huku majeruhi wakiwa ni wanne askari mmoja na raia watatu.



Askari Polisi waliofariki katika tukio hilo wametambuliwa kuwa ni  Sajini. Adam, Koplo.Peter, Koplo. Gaudin na Konstebo. Anthony.

Aidha IGP Mangu amesema mmoja wa watu waliofariki katika tukio hilo anahisiwa kuwa mmoja wa majambazi hao aliyekuwa derereva wa boda boda aliyetambulika kwa jina la Mandevu.

Kituo hicho ni Makao Makuu ya Polisi Wilaya ya Ukonga watu hao ambao idadi yao haijajulikana walivamia majira ya saa tano usiku wa Julai 12 mwaka huu na kutokomea huku wakifyatua risasi hadi barabara kuu wakiwa kwenye pikipiki na gari moja.

Mbali na kuuwa watu pia inadaiwa kuiba silaha kadhaa kituoni hapo zikiwepo SMG 15 na SR 6 na risasi.


Father Kidevu Blog inatoa pole kwa Jeshi la Polisi Tanzania na familia za wote waliofikwa na msiba huo huku iikiomba jamii kutoa taarifa za haraka juu ya wahalifu hao kwani silaha hizo zitatumika katika matukio ya kihalifu na kuleta athari klwa jamii.
Posted by MROKI On Monday, July 13, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo