MOJA ya sifa ya mwandishi ni kusoma,
na katika kusoma huko na kupekua pekua hapa na pale unaweza kujifunza na kupata
la kuandika kupitia maandiko ya watu wengine na kutoa elimu kwa umma. Leo
nimepita pita katika kurasa za marafiki zangu huko katika uso wa kitabu ‘Facebook
nikakutana na nasaha ya ndugu yangu Victory Richard, juu ya kuwasihi wanawake kwamba
sasa wavae nguo.
Ndugu yangu yule amechoshwa na tabia
za dada zetu, wake zetu na hata mama zetu wakati mwingine wanavyotembea uchi, ndio! utavaaje nguo fupiii au skintight halafu useme umevaa nguo?.
Binafsi naomba radhi kama nitakuwa nimemkwaza mtu hasa hao mama zetu, Ah! Lakini
potelea mbali Anko Kidevu sijali kitu si wamejitakia.
Hivi akina mama na dada zetu kweli
jamani katika yooote ambayo mnalilia usawa na sisi tunakubali kuwa sawa, hili
la kutembea uchi au kuvaa mavazi nusu uchi mbona mnapitiliza?
Ndio mmepitiliza Anko nimebaini kuwa
mmetupita maana sisi tukivaa sana ni kaptura au bichkoma na kawosh au singlendi
lakini sasa naona mmepita katika sketi na sasa mna vimini na kuacha vifua wazi.
Ni nani awezaye kuona aibu yenu
zaidi yangu mimi Anko Kidevu na kaka yenu Victor Richard, tafadhalini
tunawasihi, hebu vaeni nguo sasa na jamii itawaheshimu maana hakuna heshima kwa
mwanamke hata kidogo. Na kama mnahisi mnaheshimika kwa hilo ni bure kabisa.
Hivi sasa thamani ya mwanamke haipo
tena hapa nchini kwetu hasa mijini, sijui huko kwa wenzetu maana hapa nchini
hivi sasa ili mwanamke aonekane katika jamii lazima avue nguo, akitaka aonekane
mshereheshaji mzuri lazima avue nguo, ili uonekane wewe ni mwigizaji bora au
mwimbaji bora lazima uvue nguo, na ili uonekane mzuri lazima uvue nguo.
Nini hasa mnakitafuta jamani ninyi
wana wa adama? Unajua mimi nilianza kuona zamani thamani yenu inashuka tangu
nilipoanza kuona nguo zenu za ndani zikiuzwa hadharani madukani.
Kweli kabisa hazadharani!! Mlipoona
ya madukani haitoshi mkaamua sasa mkizivaa zionekane pia na kujichoresha maungo
yenu. Wengine mikorogo imewaharibu imebaki michirizi kama shamba lililovunwa
mpunga kule Kinyenze.
Unajua zamani kukuta muuza duka
ametundika nguo ya ndani ya kike anaiuza ili kuwa nadra! Lakini zile VIP zetu
zilikuwa hadharani unaziona hata ukienda duka la pipi, lakini sasa naona mambo
yamaebadilika, nguo za kiume huzioni zikiwekwa wazi madukani bali hizo zenu
kwanza ndio kivutio mlangoni, acheni bwana tumechoka inatosha.
Hivi na nyie serikali mpo wapi sasa
maadili mnaanzia kuyalinda wapi? Au katika m,ashindamno ya umiss tu lakini huku
mtaani hakuna? Sijui ni wizara gani mnahusika au ni idara ya Utamaduni?
Mnaonaje na nyie mkianza kamata kamata kama ya boda boda ukiingia mjini na
kimini au skini taiti ndani ya karandinga hao mahakama ya sokoine fine au jela.
Kwanza jiji kwa taarifa yenu
nshawapa dili la kukuza mapato yenu au idara yaUtamaduni pale kwa mama yangu
Dk. Fenela Mukangara mtakuwa mmejiongezea kipato.
Unajua hivi sasa magazeti, kurasa za
mitandao yua kijamii inayosomwa sana ni ile iliyo na picha zenu za uchi? Hili
ndo limepawa ukilema baadhi ya waandaji wa majarida na filamu ili bidhaa zao
zionekane bora na zipate soko lazima mwanamke avuliwe nguo.
Wamama zetu ndio waandaaji wakubwa
wa shughuli za kuwatoa wali au watoto ndani ni nyie ajabu mnaalika vikundi vya
wamama wenzenu wa kucheza uchi ili shughuli inoge.
Umama na udada wenu umegeuzwa kuwa
bidhaa. Wenye kupaza sauti wamekaa kimya si kwamba hawalioni hili la hasha....wengi
wao ni wanawake wanaogopana, yuko wapi mama yangu Hellen Kijo Bisimba na dada
yangu Ananilea Nkya wanaharakati wa haki za binadamu je hamuoni haja ya
kuanzisha harakati za kupinga wanawake wanao vaa nguo za kulalia barabarani?.
Ama mwaogopa mkipaza sauti juu ya hili mkaa uchi atamuhukumu siku ikifika.Sijui
naawachia ninyi.
Napongeza wizara ya mambo ya Ndani
ya Nchi pale msichana amevaa uchi haingii, kanguo kako ka kubana huko huko.
Hebu nanyie katika ofisi zenu igeni basi.
kwanza kabisa, duniani mwote hakuna mtu/mwanadamu awezaye kutembea uchi bila ya kukaliwa na roho chafu/mapepo - kumbuka adamu na hawa walivyojigundua wa uchi.
ReplyDeletewapo wanawake wa aina mbili
1. wanaojilazimisha kutovaa nguo mpaka mapepo maimuna yanawaingia na kufanya tabia ndani mwao
2. wale ambao kwa asili kutokana na mapokeo wana roho tu chafu na hivyo hiyo ni tabia
marekebisho ya kiroho yanatakiwa kwa wanawake ili washinde hali hizi