Na
Fadha Kidevu Blog
MABINGWA wa soka Tanzania bara
wameingia mkataba wa miaka miwili na Benki ya NMB jana
Kwa mujibu wa Mweyekiti wa Azam Said
Mohamed alisema mkataba huo utakuwa ikiisadia timu hiyo mambo mbalimbali
ikiwemo vifaa vya michezo kama Jezi,Viatu na nauli ya kusafiria wakati wa mechi
za mikoani.
“Udhamini wetu na NMB,utakuwa ukihusisha vifaa vyote vya michezo ikiwemo
Jezi,Viatu na vifaa vingine na hatuwezi kusema gharama yake kwa sababu ni
makubaliano yetu sisi na NMB ,”alisema Mohamed.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji
wa NMB, Mark Wiessing alisema mafanikio ya Azam FC pamoja na uongozi bora
ndivyo vilivyo wavutia kuingia nao mkataba huo ambao anaamini utakuwa na
manufaa kwa pande zote mbili.
Hiyo siyo mara ya kwanza kwa NMB kujiingiza
katika udhamini wa michezo mara ya kwanza iliwahi kuidhamini timu ya taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars,mwaka 2007 hadi 2010 na imekuwa ikitoa mchango katika
kuendeleza soka la vijana nchini.
0 comments:
Post a Comment