Nafasi Ya Matangazo

November 08, 2012

Shiliningi milioni 5 za kitanzania zinahitajika ili kuwanusuru watu wawili walionasiana wakivunja amri sita.

Watu wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam wanadaiwa kukutwa wakiwa wamenasana wakati wakifanya tendo maalum la watu walio katika mahusiano (mke na mume) na kwakua wao sio mke na mume halali wamenasiana. 

Mume wa mwanake ambae amefikwa na maswaibu hayo ya mwaka jijini Dar es Salaam anahitaji kiasi hicho cha fedha ili atoe PASSWORD ya pin hiyo kali aliuyoiweka katika eneo takatifu la unyumba wao.

 Taarifa za awali kutoka Temeke zinapasha kuwa wawili hao wapo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa unasuaji ambao wadadisi wa mambo hasa ya kijamii wanadai Hospitali hawataweza kuwanasua isipokuwa kwa wataalm wa jadi hasa Mume wa Mwenye mke ambaye aliwekewa tego. 

Blog hii itatujuza zaidi juu ya tukio hilo ambalo hadi sasa limekuwa ni gumzo jijini na kujaza umati mkubwa wa watu na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu eneo la tukio.  

WAKATI HUO HUO taarifa yake Kamanda Mwaikenda inaeleza kuwa ; UVUMI umezagaa jijini Dar es Salaam leo, kwamba mwanaume na mke wa mtu wamenasana wakifanya mapenzi kwenye gesti moja wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Tukio hilo lililoanza kusikika asubuhi, lilisababisha tafrani kubwa zilianza kusikika jana asubuhi  ambapo watu walijazana katika Hospitali ya Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na hamu ya kutaka kuwaona wapenzi hao.

Polisi walipata wakati mgumu kuwatawanya watu hao, waliokuwa wamefurika ndani na nje ya  katika Hosptali ya Temeke, wakipiga kelele kuwataka wauguzi na madaktari wawaoneshe wapenzi hao ambao hata hivyo majina yao hayakuweza kujulikana.

Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliamua kupiga mabomu kuwatawanya watu ambao wengi wao walikuwa wabishi wakitaka waendelee kuwepo eneo hilo kwa lengo la kutaka kuwaona wapenzi hao wanaodaiwa kunasana.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Aman Malima alikanusha kuwepo kwa tukio la kunasana kwa mwanamke na mwanaume kinyume cha maumbile.

Dk. Malima aliwasihi wanahabari na wananchi kuondoka eneo la hospitali ili waendelee na kati ya kuwahudumia wagonjwa. Baadhi ya huduma zilisimamishwa kwa muda hospitalini hapo.

Baadhi ya wananchi waliokaidi kuondoka eneo hilo na kubaki kuchungulia kupitia kwenye nondo za uzio wa hospitali hiyo walisikika wakipiga kelele wakitaka jeneza linalotumika kubebea maiti hospitanini hapo, ambalo lililkuwa nje ya mochuari, lifunuliwe ili waone maiti ya mwanamke aliyehusika katika sakata hilo waliyeambiwa kuwa amekufa.

Akizungumza na Jambo leo mmoja wa mashuhuda hao Juma Said (32)mkazi wa Kigogo, alisema tukio hilo ni la kweli kwani yeye ameona kwa macho yake hajasimuliwa.

"Asubuhi watu wasiofahamika na kutojulikana wametoka wapi wameshushwa katika gari la polisi katika Hospitali ya Temeke huku wakiwa wamenasana kinyume na maumbile," alisema Said.

Alisema watu hao walikuwa wamefunikwa na shuka jeupe na kuingizwa ndani ya Hospitali hiyo.

"Watu hao nimewaona mwenyewe kwa macho yangu wakiwa wamenasana kinyume cha maumbile huku mwanamke huyo akiwa amechoka sana kwamuonekano wake," alisema.

Said anasema kwa taarifa walizoendelea kuzipata baada ya watu hao kuingizwa hospitalini hapo zinadai kuwa mwanamke amefariki dunia.

Wakati huohuo mfanya biashara wa maeneo hayo ambaye hakutaka jina lake litajwe katika gazeti alidai watu hao ni kweli wamefikishwa katika Hospitali hiyo majira ya asubuhi.

Mfanyabiashara huyo alisema watu hao wameshushwa Hospitalini hapo wakiwa wamenasana kinyume na maumbile huku wakiwa wamefunikwa shuka jeupe.

"Watu hao ni wapangaji wa nyumba moja, mwanamke aliagwa na mume wake ambaye ni dereva wa magari makubwa kwamba anakwenda Tanga kikazi hivyo mke akapata muda wa kutoka na mpangaji mwenzie ambaye pia ni mume wa mtu ndipo walipokumbana na tukio hilo," alisema mfanyabiashara huyo.

Alisema baada ya tukio hilo ndugu wa mwanamke waliamua kupiga simu kwa mume wake ambaye alimuaga kuwa anaenda Tanga kikazi na kumjulisha yaliyotokea ambapo mume alisema anataka faini ya sh. million tano kutoka kwa mwanaume aliyekutwa na mkewe ndipo awatenganishe.

 Wananchi wakiwa wamefurika katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam leo, wakiwa na hamu ya kutaka kuwaona mwanaume na mke wa mtu waliodaiwa kunasana wakifanya mapenzi katika moja ya nyumba za kulala wageni wilayani Temeke.
 FFU wakipiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliofurika Hospitali ya Hospitali ya Temeke
 Baadhi ya watu waliofurika upande wa Hospitali ya Taifa Muhimbili waktaka kuwaona wapenzi walionasana
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk. Aman Malima akishangaa kuona umati huo. Alikanusha kuwepo uvumi huo
vijana wakishabikia kutaka kuwaona.
Posted by MROKI On Thursday, November 08, 2012 5 comments

5 comments:

 1. VIOJA VYA WALIMWENGU

  ReplyDelete
 2. KUKOSA KAZI SASA KAMA WAMEGANDANA INAWASAIDIA NINI WAKIONA. TZ BWANA OVYO HASA DAR

  ReplyDelete
 3. KWNNZA: Picha ya kwaza ni ya ishu ya zamani huko Kenya

  THerefore hata picha zingine inawezekana ni matukio tofauti umetuwekea humu hayahusiani na mkasa husika.

  PILI: Humbu kwenye habari unasema mara TMK mara Muhimbili, bila kuunganisha kua ishu imetokaje TMK hadi sasa inakua Muhimbili.

  JUMUISHO: Hii habari kama sio ya uongo basi ina maswali mengi kulio majibu

  ReplyDelete
 4. Habari yote hiyo ni uongo mtupu,hata picha ya wapenzi
  yenyewe haieleweki. Watanzania hawana kazi za kufanya hadi waamkie kuona waliogandana! Ili iwasaidie niniaaaaaaa?

  ReplyDelete
 5. Mwandishi wa ahabari ana kasoro kubwa sana,kwanza maelezo yake yanaonekana ya kubuni zaidi, picha ya watu anaowadhani wameganadana ni picha ya tukio lililotokea kenya ambayo vedio yake pia inapatikana kwenye mtandao. kwa iyo inawezekana hata hizo picha nyengine si ktk tukio anlozungumzia.

  ReplyDelete

 • Facebook
 • Twitter
 • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo