Nafasi Ya Matangazo

June 12, 2012

 Wakazi wa Eneo la Ukonga Majumba Sita Wilaya ya Ilala jijini Dar es sal;aam leo walifunga barabnara kuu ya Nyerere katika eneo hilo la majumba sita kushinikiza kuwekwa kwa matuta katika eneo hilo kufuatia kukuthiri kwa ajali za wakazi wa eneo hilo kugongwa wavukapo barabara hiyo.

Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa za asubuhi na kudumu hadi saa nane mchana baada ya kijana mmoja kungongwa katika eneo hilo akijaribu kuvuka barabara hiyo na kufa papo hapo.

Wakiwa na mabango, mawe na matofali wakazi hao waname, wanawake, wazee kwa watoto walifurika katika barabara hiyo na kushinikiza kuja kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwekwa kwa matuta.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi barabarani na hata Jeshi la polisi lililopfika na kuwasihi waruhusu magari kupita waligoma na huko mitaani pia walizuia boda boda (pikipiki) kupita hadi matuta yawekwe.
 Magari yakiwa yamezuiwa eneo hilo karibu na Kambi ya Jeshi Kikosi cha Anga.
 Wananchi wakiwa upande wa pili wa barabara kutaka kujua hatma ya usalama wao.
Watu walikuwa ni wengi. Awali eneo lingine katikati ya Njia Panda segerea na Minazi Mirefu (Banana) wanafunzi wa shule ya Msingi Minazi Mirefu waliwahi kuandamana barabarani hapo kushinikiza kuwekwa kwa matuta baada ya wenzao kadhaa kugongwa na serikali ikaweka matuta hayo na hivi sasa hali ni shwari katika eneo hilo.
Posted by MROKI On Tuesday, June 12, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Kaka,

    Waliosema AJIRA ni time Bomb kweli hawakukosea.
    Yaani saa 3 asubuhi umati wote huo uliojaa hapo ina maana hao wote hawana Ajira hao!

    Duuh!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo