Rais Jakaya Kikwete leo amefunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa Mkoani Iringa. Pamoja na kuhutubia katika kilele hicho pia Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma za maji na wadau mbalimbali wa maji nchini. Pichani ni Rais Kikwete akiwa katika banda la Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo ya mwaka huu yaliyofanyika uwanja wa Samora Mjini Iringa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Meneja Uwajibikaji na Miradi Endelevu wa SBL, Nandi Mwiyombela.
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na Kupokelewa na Mkurugenzi wake wa Mahusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda. Pia SBL walipokea Cheti cha ushiriki wa maonesho hayo.
Meneja Uwajibikaji na Miradi Endelevu wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Nandi Mwiyombela,akisaliamiana na kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete katika banda la Kampuni ya Bia ya Serengeti lililopo katika viwanja vya Samora mjini Iringa yalipofanyika maonesho ya wiki ya Maji kitaifa.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika banda la Chuo Kikuu cha Tumaini lililopo katika maonesho ya Wiki ya Maji kitaifa mjini Iringa. Rais Kikwete akiwa katika banda hilo alipata fursa ya kupewa maelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tafiti ya chuo hicho kusiana na huduma ya maji na ulipaji Ankara. Aidha Rais Kikwete aliwapa ushauri chuo hicho kufanya utekelezaji wa tafiti hizo na sio ziwe zinaishia katika makaratasi tu.
Rais Jakaya Kiwete akiwa katika Banda la TAWASANET na kupata maelezo mbalimbali ya kuhusiana na mtandao huo wa watoa huduma za maji nchini.
0 comments:
Post a Comment