Nafasi Ya Matangazo

February 04, 2010

Stakabadhi ambayo Polisi, kupitia Kamnda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, walimtaka mwandishi wa habari za uchunguzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro, kuionesha imepatikana.

Hali hiyo inajitokeza baada ya kile alichoapa Kova kwamba hakuna raia anayeweza kumiliki pingu, na kwamba alikuwa na hakika kwamba Muro asingeweza kupeleka risiti hiyo.

Juzi akiendelea na juhudi zake za kuwakamata watuhumiwa na kuwahukumu huku akisema wengine ni “matapeli sugu”, Kova alisema kwamba Muro aliyekamatwa Jumapili iliyopita na kuachiwa kwa dhamana, alikuwa hajawasilisha risiti hiyo.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kwamba Muro alinunua pingu hiyo kihalali kutoka duka la kuuza silaha la Shirika la Mzinga. Shirika hili ni mali ya serikali.

Risiti aliyopewa Muro ni moja ya ushahidi wa ununuzi wa pingu hiyo, ikiwa na namba 34357310. Stakabadhi hiyo ni mali ya serikali pia.

Risiti hiyo iliyotolewa Mei 20, mwaka 2008, inaonyesha kuwa Muro alinunua pingu kwa Sh, 25,000. Muro ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, Jumapili iliyopita alikutwa na pingu katika gari alilokuwa akilitumia mara baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kutaka fedha kwa njia ya vitisho kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.
Posted by MROKI On Thursday, February 04, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo