Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2026



Madereva wa pikipiki maarufu bodaboda katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mizengo Pinda, mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kujilinda wao wenyewe pamoja na abiria wanaowahudumia.

Elimu hiyo imetolewa Oktoba 13, 2026 na Sajenti wa Polisi Veronica Rumisha, ambapo amewasisitiza madereva hao umuhimu wa kuvaa kofia ngumu (helmet) kila wanapotumia pikipiki, akieleza kuwa kofia hiyo husaidia kupunguza madhara ya majeraha makubwa kichwani yanayoweza kutokea wakati wa ajali.

Aidha, Sajenti Rumisha aliwataka kuacha tabia ya kuendesha kwa mwendokasi, kuzidisha idadi ya abiria maarufu kama mshikaki bali wabebe idadi ya abiria inayoruhusiwa kisheria pamoja na kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za kujipatia kipato.


Posted by MROKI On Tuesday, October 13, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo