RC Chalamila ameyasema hayo leo Mei 20, 2026 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere Terminal 3 wakati akiiaga team hiyo kuelekea Kigali Rwanda kwenye mashindano.
Aidha RC Chalamila ametoa rai kwa wakazi wa Mkoa huo endapo watabaini kuna kijana anakipaji cha basket ball,wamlete ofisini kwake ili aweze kuendelezwa kipaji hicho pamoja na kumuunganisha na wachezaji nguli wa Dar City Basket Ball.
Vilevile RC Chalamila amesema Rais wa team hiyo Ndg Hashimu Thabit akirudi toka Rwanda uandaliwe utaratibu wa kukutana na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa Mkoa huo kuona namna ya kuwa na uwanja mkubwa wa kisasa wa Basket Ball katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amesema Dar City ni team ya kimataifa na inafanya vizuri ni ya kihistoria toka Tanzania ipate uhuru hivyo anaitakia kila kheri.
Mwisho RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya michezo kwa kuwa michezo ni afya lakini pia michezo ni uchumi.















0 comments:
Post a Comment