Nafasi Ya Matangazo

January 29, 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Huduma ya Ugavi na Ununuzi wa Ofisi hiyo, Bi. Juliana Mkalimoto (katikati) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake alipotembelea ofisi hiyo. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akipata maelezo kuhusu maendeleo ya ukarabati wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa jengo hilo, Bw. Paul Laizer wakati wa ziara yake alipotembelea ofisi hiyo. 

Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ukarabati wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam, Bw. Paul Laizer akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi kuhusu maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo wakati wa ziara ya Dkt. Muyungi kujionea maendeleo ya ukarabati huo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa amekaa katika moja ya viti vilivyopo katika jengo la ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ukarabati wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam, Bw. Paul Laizer akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi kuhusu maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo wakati wa ziara ya Dkt. Muyungi kujionea maendeleo ya ukarabati huo.
*************************
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi ameeleza kuridhishwa kwake na ukarabati wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya ziara yake ya kukagua jengo hilo, Dkt. Muyungi ameipongeza kamati ya usimamizi wa ukarabati wa jengo hilo kwa kumsimamia vyema mkandarasi kukamilisha kazi hiyo inakamilika katika wakati na muda uliopangwa.

“Niwapongeza kamati ya ukarabati wa jengo hili kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya, jambo muhimu ni kuhakikisha marekebisho madogo madogo niliyoyaona yanafanyiwa kazi ili tuweze kukabidhiwa jengo hili” amesema Dkt. Muyungi.

Aidha Dkt. Muyungi ambaye katika ziara hiyo aliongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya ukarabati wa jengo hilo, Bw. Paul Laizer amesifu mfumo wa miundombinu ya TEHAMA iliyofungwa katika jengo hilo ambayo itarahisisha utendaji kazi kwa viongozi na watumishi.

Ameeleza kuwa katika ziara hiyo pia amejionea maboresho makubwa yaliyofanywa na kutoa maelekezo kwa mkandarasi kuhakikisha anafanyia kazi maoni na ushauri alitoa ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati  ili kuweza kutumika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa ukarabati wa jengo hilo, Bw. Paul Laizer amemhakikishia Dkt. Muyungi kuwa kamati yake ushauri, maoni na mapendekezo yanafanyiwa kazi ili kuwezesha kukamilika kwa jengo hilo.
Posted by MROKI On Thursday, January 29, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo