Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mvomero kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Sara Msafiri Ally, ameendelea na kampeni zake katika Kata ya Msongozi na Doma.
Katika mikutano yake na wananchi, Bi. Sara aliwaahidi kuwa endapo atachaguliwa pamoja na Rais na Diwani wa CCM, watahakikisha miundombinu ya wakulima inaboreshwa ili kurahisisha kilimo cha kisasa. Vilevile, aliwahakikishia wafugaji kuwa serikali itawaongezea maeneo ya kufugia pamoja na kuboresha mbegu za mifugo ili kufanikisha ufugaji wenye tija.
Aidha, alimnadi mgombea urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa Rais ameahidi kuongeza ndege kwa ajili ya kufukuza tembo wanaosababisha usumbufu kwa wananchi vijijini.
Katika hotuba yake, Bi. Sara pia aliwakumbusha wananchi kuwa serikali ya CCM tayari inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa bwawa jipya linalojengwa Morogoro Vijijini, mradi utakaohakikisha wananchi wa Mvomero wanapata maji safi na salama.


















0 comments:
Post a Comment