Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, amesema Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme na kudunisha ushirikiano uliowekwa na waasisi wa nchi hizo.
Mhe Kapinga ameyasema hayo leo tarehe 20 Machi,2025, mkoani Pwani wakati alipofanya ziara katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Waziri Badir na ujumbe wake.
‘’ Tunamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa msingi imara wa utekelezaji wa miradi huu wa umeme na tumeona matunda halisi ya usimamizi wake.’’ Amsema Mhe.Kapinga
Amesema nchi ya Misri imetekeleza mradi huo wa JNHPP kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya Tanzania ambapo mpaka sasa mashine nane kati ya tisa zimewashwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa JNHPP, Waziri, Dkt Badir Abdelatty, amesifu ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuishukuru Tanzania kwa kuiamini nchi yake kutekeleza mradi huo wa JNHPP, kwani utawanufaisha wananchi wa Tanzania walio wengi hususani wale wanaozungukwa na eneo la mradi.
Amesema nchi za Afrika zinapaswa kujivunia uwepo wa miradi ya umeme kwa maendeleo ya waafrika wenyewe na kuahidi kuwa Misri itaendeleza ushirikiano na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi mingine kama hiyo
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo amesema, Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ulionao ili kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi hususani kwenye miradi ya sekta ya Nishati
Ziara hiyo.imehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri….., Balozi wa Misri nchini Tanzania, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta, Dk James Mataragio, na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment