Nafasi Ya Matangazo

March 21, 2025

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Moshi Jonathan Kabengwe amesema majina ya waombaji wa ajira 1,596 za TRA zilizotangazwa hivi karibuni yatatangazwa rasmi Machi 22.2025 kupitia tovuti ya www.tra.go.tz kwa ajili ya usaili wa kuandika utakaofanyika Machi 29 na 30 mwaka huu kwenye vituo 9.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo tarehe 21.03.2025 Bw. Kabengwe amesema kati ya waombaji 135,027 waliotuma maombi ya nafasi za ajira, waombaji 112,952 wamekidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili wa kuandika.

Amesema kila muombaji atatumiwa taarifa ya kuitwa kwenye usaili katika barua pepe yake aliyoiambatanisha kwenye maombi ya kazi na kuwa waombaji wenye mahitaji maalum wamewekewa utaratibu maalum ambao utawasaidia kufanya usaili bila usumbufu.

Bw. Kabengwe amesema usaili huo utafanyika kwenye Mikoa 8 na Zanzibar ambayo ni
1. Dar es Salaam ambayo itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na
Pwani;
2. Zanzibar ambayo itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba;
3. Arusha ambayo itahusisha waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga;
4. Dodoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora;
5. Mtwara ambayo itahusisha waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma;
6. Mbeya ambayo itahusisha waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa;
7. Mwanza ambayo itahusisha waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu;
8. Kagera ambayo itahusisha waombaji kutoka Kagera na Geita; na
9. Kigoma ambayo itahusisha waombaji kutoka Kigoma na Katavi.

Bw. Kabengwe amebainisha kuwa waombaji wote watatendewa haki.
Posted by MROKI On Friday, March 21, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo