Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akitoa vyeti kwa Wahitimu Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024.
Matukio Mbalimbali Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KATIKA kuimarisha huduma za afya serikali inaendelea na juhudi za ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu na huduma za afya katika hospitali zote kuanzia ngazi za chini hadi hospitali za rufaa.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga Katika mahafali ya sita ya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Excellent yaliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani leo Desemba 12, 2024. Amesema kuwa serikali imejipanga vyema ili kuhakiisha kwamba inakuwa na vifaa bora na vya kisasa kwaajili ya kujifunzia na kutoa huduma za afya katika ngazi zote nchini.
"Maono ya Rais Dkt. Samia hayawezi kuwa na tija kama kutakosekana wataalamu wa kufanya kazi ndio maana nawapongeza kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita kwa kuzalisha wataalamu wasaidizi katika fani Utabibu, Uuguzi, Ukunga, Famasia na wataalamu wa Maabara.
"Juhudi zenu tunazijua na tunazitambua ndugu zanguni endeleeni kuzingatia ubora maana wahitimu hawa si kwamba wanakwenda kuokoa maisha ya watu wetu bali hata sisi hapa ni wateja wao tunaomba muwapokee mtakapokuwa huko makazini"
Akijibu risala ya Mkuu wa Chuo hicho, Kipanga amesema kuwa atawasiliana na TAMISEMI pamoja na TARURA ya Mkoa wa Pwani ili kuona namna bora ya kuboresha miundombinu ya barabara ya kufika hapa chuoni na katika kampasi nyingine kama zilivyoandikwa kwenye risala.
Pia ametoa wito wa wahitimu hao kuonesha weledi katika kazi kwasababu kusoma ni jambo jingine na kufanya kazi ni jambo jingine, unaweza ukasoma lakini usielimike.
"Wito wangu kwenu ni kahakikisha yale ambayo mmeyapata mnakwenda kuyatumia pale mnapoenda kufanya kazi kwa weledi." Amesema Kipanga
Pia amewaasa kuepuka masuala ya rushwa ufisadi na kujikinga na magonjwa mbambali kwani taifa linawahitaji sana.
Aidha amesema ni muhimu mkafahamu kwamba elimu haina mwisho kimsingi wanavyosheherekea mahafali wajuae kwamba wamefungua njia ya kuendeleza taaluma waliyopata hadi wawe wataalamu bobezi katika fani zao.
Kwa Upande wa Mkuu wa Chuo, Kelvin Kenan ameiomba serikali kuwasaidia kutengeneza miundombinu ya barabara itakayofika chuoni hapo ili kuchochea maendeleo zaidi katika chuo hicho.
Kwa upande wa Wahitimu wa Chuo hicho wamewashukuru wakufunzi wao lakini pia wameomba kuwepo na bajeti za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ili kuweza kupata elimu bora.
Pia wameiomba serikali kuwapatia mikopo wanafunzi wa vyuo vya kati kwani changamoto kubwa ni kutokuwa na fedha za kujikimu kimaisha wawapo chuoni.
Licha ya hayo wameomba kuwe na fursa ya wahitumu wa chuo hicho kwenda kusoma nje ya nchi kama ilivyo vyuo vikuu vingine.
0 comments:
Post a Comment