Nafasi Ya Matangazo

November 10, 2024

Jumla ya watahiniwa 7176 waliosajiliwa katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela wataungana na watahiniwa wenzao nchini kote kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2024 utakaoanza tarehe 11 hadi 29 Novemba 2024.

Taarifa kutoka ndani ya Halamashauri hiyo na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Violencea S. Mbakile imefafanua hayo.

Kati ya watahiniwa hao wavulana ni 3467 na wasichana ni 3709 watafanya mtihani huo, ambapo watahiniwa 6989 ni watahiniwa wa shule wasichana wakiwa 3588 na wavulana wakiwa 3401. 

Na watahiniwa wa kujitegemea wapo 187 wavulana wakiwa 66 na wasichana wakiwa 121 watafanya mtihani huo wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2024.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla ya vituo 60 vilivyo sajiliwa kuendesha mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) kwa mwaka 2024, kati yake vituo 48 ni vya watahiniwa wa shule na vituo 12 ni vya watahiniwa wa kujitegemea.

Mkurugenzi Ummy Wayayu, kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, anawaombea na kuwatakia kila la kheri watahiniwa wote wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2024 na kuwakumbusha kuzingatia na kufuata taratibu zote za mitihani ili waweze kuhitimu salamm. 
Posted by MROKI On Sunday, November 10, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo