Simba ameyasema hayo katika kikao kazi na wahariri na waandishi wa vyombo ya habari nchini, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR). Kilichofanyika leo Novemba 4,2024 Jijini Dar es Salaam.
Amesema kupitia mfumo huo wazabuni zaidi ya 28,590 wamejisajili huku mikataba ya zabuni 62,267 yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 10.2 imetolewa nakwamba hadi kufikia Oktoba 31, 2024 jumla ya taasisi za ununuzi 21,851 zimesajiliwa na zinatumia Mfumo wa Kielektroniki (NeST).
"ununuzi wa umma ni shughuli muhimu ya kiuchumi inayohusisha sehemu kubwa ya Pato la Taifa (GDP) takribani asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali na taasisi zake hutumika kwenye ununuzi wa umma, hivyo ununuzi wa umma nchini unasimamiwa na Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410." "Chini ya sheria hii zimeundwa Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 na miongozo kwa ajili ya kuweka taratibu za ununuzi wa umma. Kanuni mpya za Ununuzi wa Umma zimekwishakamilika." amesema Simba.
Pia amesema kuwa Mamlaka hiyo imewezesha ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa umma na kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa wananchi kwa kuanzisha kanda sita katika mikoa ya Mwanza, Dar es Saalam, Arusha, Mbeya,Tabora na Mtwara.
Ameongeza kuwa zabuni zenye thamani isiyozidi shilingi bilioni 50 zimetengwa kwa ajili ya wazabuni wa ndani ya nchi pekee nakwamba mumo wa NeST unaisaidia PPRA katika kulisimamia hilo kwa ufanisi zaidi.
“Tuwapongeze kwa kurahisisha mfumo wa ununuzi katika nchi yetu, ndugu zangu wahariri, hata matangazo ya kwenye vyombo vya habari mengi yanapitia NeST, kwa hiyo sisi tunaoendesha vyombo vya habari kama huna akaunti ya NeST huwezi kufanikisha matangazo, hali ngumu ya vyombo vya habari tuliyonayo tuna nafasi ya kujikomboa kupitia kwenye mfumo huu” amesesema Bw. Balile.
PICHA ZA WAHARIRI KATIKA MKUTANO HUO
0 comments:
Post a Comment