Nafasi Ya Matangazo

November 08, 2024


🔴Asema Taasisi zinazotoa huduma kwa jamii zinapewa kipaumbele

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema asilimia 99 ya Vijiji vyote nchini vimefikiwa na nishati ya umeme. 

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Novemba 08, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Rehema Lugangira aliyeuliza iwapo Serikali haioni haja ya kupitia upya mkataba wa REA ili kuifanya  iwe na jukumu la kufikisha umeme kwenye vituo vinavyotoa huduma.

"Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendela na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kupeleka umeme Vijijini ambapo hadi kufikia mwezi Oktoba, 2024 takriban asilimia 99 ya vijiji vyote vimefikiwa na nishati ya umeme." Amesema Mhe. Kapinga  

Ameongeza kuwa, utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini unatoa kipaumbele katika  taasisi zinazotoa huduma kwa jamii zikiwemo shule, vituo vya afya, zahanati, pampu za maji na taasisi za dini ili kuboresha utolewaji wa huduma kwa wananchi. 

Amesema hadi kufikia mwezi Septemba 2024, taasisi za kijamii zilizopatiwa umeme kupitia REA ni; taasisi za elimu- 12,905, taasisi za afya- 6,768, pampu za maji- 5,872, nyumba za ibada -8,822 na maeneo ya biashara ni 29,294.

Aidha, amesema Serikali itaendela kuisimamia REA ili kuhakikisha inatoa kipaumbile kwenye upelekaji wa umeme kwenye Taasisi  za umma pale inapokuwa imekamilisha miradi ya usambazaji wa umeme vijijini.

Akijibu swali kuhusu kufanana kwa gharama ya kuunganisha umeme kwenye nyumba ambayo ina umeme na isiyokuwa na umeme, Mhe. Kapinga amesema gharama za msingi za kuunganisha umeme kwenye nyumba zinahusisha gharama ya mita, waya pamoja na gharama ya kazi ambazo hazibadiliki.
Posted by MROKI On Friday, November 08, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo