Meneja wa Idara ya Kuweka Akiba na Kukuza Uchumi wa Kaya wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Sarah Mshiu, akipokea tuzo ya kutambua mchango wa TASAF katika kukuza uchumi kwa wananchi kutoka kwa Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaka wakati wa hafla ya kufunga wiki ya huduma za fedha iliyofanyija kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe jinini MbeyaMbeya kushoto ni Melkizedeki Nduye Afisa Mawasiliano wa TASAF.
Meneja wa Idara ya Kuweka Akiba na Kukuza Uchumi wa Kaya wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Sarah Mshiu, akipokea tuzo ya kutambua mchango wa TASAF katika kukuza uchumi kwa wananchi kutoka kwa Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja wakati wa hafla ya kufunga wiki ya huduma za fedha iliyofanyija kwenye viwanja vya Rwanda Nzovwe jinini Mbeya, kushoto ni Meleckzedeck Nduye Afisa Mawasiliano wa TASAF.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Meneja wa Idara ya Kuweka Akiba na Kukuza Uchumi wa Kaya wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Sarah Mshiu, amempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutambua na kuunga mkono juhudi za TASAF katika kuboresha maisha ya kaya za walengwa nchini.
Akizungumza leo, Oktoba 26, 2024, baada ya kufungwa kwa Maadhimisho ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika jijini Mbeya, katika viwanja vya Rwanda Nzovwe, Mshiu alieleza kuwa Mpango wa TASAF unalenga kuwainua kiuchumi kaya maskini kwa kuwapatia fursa za kuweka akiba na kukuza kipato kupitia miradi midogo midogo.
“Tunaichukulia Wiki ya Huduma za Fedha kama fursa muhimu ya kuwafikia walengwa wetu na kuwashirikisha katika shughuli za kifedha. Tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za TASAF za kutoa msaada wa kifedha na elimu kwa walengwa ili kuwawezesha kujimudu kiuchumi,” alisema Mshiu.
Aidha, Mshiu alibainisha kuwa TASAF imeendelea kutoa mchango mkubwa katika kusaidia kaya maskini, ambapo ushiriki wao katika maadhimisho hayo umewaletea tuzo na zawadi mbalimbali kwa kutambua mafanikio ya programu hiyo.
Safiri Luaga, mmoja wa wanufaika wa TASAF kutoka Kata ya Iziwa, Mbeya, alieleza kuwa kupitia msaada wa TASAF, yeye na wenzake wameweza kuunda kikundi cha watu 12, wakiwemo wanaume wawili na wanawake kumi, ambacho hukutana kila Jumatano kwa ajili ya kuweka akiba na kutoa mikopo midogo midogo kwa wanachama.
“Kikundi chetu hukutana kila Jumatano, na tunachangia shilingi 1,000 kila mmoja. Tunakopesha shilingi 10,000 na kurudisha shilingi 10,500. Kutokana na mikopo hii, tumeweza kujenga uwezo wa kiuchumi na kuhudumia familia zetu. Hii yote ni kwa msaada wa TASAF,” alisema Luaga aliyeshiriki maonesho hayo.
0 comments:
Post a Comment