Nafasi Ya Matangazo

October 19, 2024




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze amefika kijijini kwao Msoga, Chalinze kujiandikisha ikiwa ni kutimiza takwa la katiba la kujiandikisha ili apate nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024. 

Akizungumza baada ya kumaliza kujiandikisha , Mh. Kikwete amepongeza sana utulivu katika kipindi hiki cha uandikishaji. “…. Amani ni tunu yetu, na muhimu kujitambulisha nayo kwa vitendo na Watanzania wanathibitisha hili kwa vitendo”, alisema Waziri Kikwete. Pamoja na kuwapongeza Watanzania kwa utulivu pia alishukuru Serikali kwa kuamua kuongeza vituo vya kujiandikisha kutokana na wananchi kulalamika kutembea umba mrefu kufuata kituo cha kujiandikisha. Waziri Kikwete alisema, “…. Naishukuru na kuipongeza Serikali kwa maamuzi ya kutuongezea kituo. Kuna watu wanatoka Chalinze mzee, Chahua walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata kituo cha kujiandikisha. Lkn kwa maamuzi haya tunataraji namba itaongezeka na matarajio ya wananchi kupata haki yao ya kupiga kura yapatikana. Nakupongeza msimamizi kwa niaba ya tume na serikali. “

Zoezi hili ambalo lilizinduliwa tarehe 11 na Mh. Rais limekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa halmashauri ya Chalinze imefikia zaidi ya 80 na wanaendelea huku kimkoa, wilaya ya Mkuranga ikiendelea kufanya vizuri katika uandikishaji.

Wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki wamesifu, taratibu zilizoandaliwa na usimamizi na sasa wako tayari kwa zoezi lililombele la kuchagua viongozi wa serikali.
Posted by MROKI On Saturday, October 19, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo