Nafasi Ya Matangazo

October 09, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ruzuku ya bei kwenye mitungi ya gesi inayotolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili Watanzania watumie nishati safi na salama kwa afya zao pamoja na kuhifadhi mazingira nchini. 
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu, Mha. Advera Mwijage wakati akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Gairo na wananchi mara baada ya kutembelea banda la REA kwenye Maonesho ya Samia KILIMO Biashara Expo 2024 yanayofanyika katika wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

"Mhe. Rais Samia ametoa ruzuku ya bei kwenye mitungi ya gesi ili iuzwe kwa bei rafiki, kusambazwa kwa wingi na kila Mtanzania aimudu na atumie nishati hii muhimu," Amesena Mha. Mwijage. 

Aidha, REA itaendelea kusambaza kwa wingi majiko ya gesi nchini na wilaya ya Gairo pekee jumla ya majiko 3,225 ya gesi yatatolewa kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuitangaza na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. 

Ameongeza kuwa, REA wameanza kutoa majiko banifu 790 kwa wananchi wa Gairo ambayo ni majiko rafiki, imara REAukwa muda mrefu, yanatunza mazingira na yanatumia kiasi kidogo cha mkaa. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku ya bei kwenye mitungi hiyo kwa wananchi wake ambapo itarahisisha upatikanaji wake kwa wingi.

"Wananchi wenzangu wa Gairo, majiko haya ni rafiki kwa matumzi, salama kwa afya zenu, ni msaada mkubwa katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira yetu. Nawahimiza kuyanunua ili nishati hii iwe na manufaa makubwa kwenye familia zetu badala ya kuendelea kukata miti kupata mkaa na kuni, " Amesema Mhe. Makame.

Wananchi wa Gairo na maeneo jirani ya wilaya hiyo wameendelea kufurahia ruzuku ya bei ya majiko ya gesi na majiko banifu na kuipongeza Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo na kuwataka ambao hawajapata majiko hayo kutembelea banda la REA.



Posted by MROKI On Wednesday, October 09, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo