Nafasi Ya Matangazo

October 17, 2024

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Watumishi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la Mpiga Kura, ili watumie haki yao kupiga kura na kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.

Kaulihiyo, imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, ambaye amewahimiza watumishi wa taasisi yake, ambao wapo kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mha. Besta pia amehimiza kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, ili  wakachague viongozi wenye kusimamia maendeleo kama vile maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa.

“Naendelea kuhimiza kwa kuwa zimebaki siku chache basi watumishi wenzangu mhakikishe mnakwenda kujiandikisha na mwisho siku ya kupiga kura napo mkapige kura kwa kuchagua viongozi bora wenye kutuletea maendeleo katika maeneo yetu,” amesisitiza Mha. Besta.

Zoezi la uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Mpiga Kura linaendelea nchi nzima ambapo lilianza tarehe 11 hadi 20 Oktoba, 2024, ambapo kaulimbiu ni “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi” .
Posted by MROKI On Thursday, October 17, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo