Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongoza kikao cha
Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) cha kujadili masuala
ya Muungano kilichofanyika jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan
Juma, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) na
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Salhina Mwita Ameir.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) akishiriki kikao cha Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi SJMT na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma. Wengine kuanzia kulia ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile.
Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakishiriki kikao cha Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na SMZ kilichofanyika jijini Dodoma kuanzia kushoto Waziri wa Nchi Ofisi Rais (Fedha na Mipango) Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo.
Wataalamu kutoka Wizara za
Kisekta na Taasisi mbalimbali za wakishiriki kikao cha Kamati ya Pamoja ya
Fedha na Uchumi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma
0 comments:
Post a Comment