Nafasi Ya Matangazo

October 11, 2024

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.

Bi. Kwakwa alilakiwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, Ofisini Kwake  Jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (kushoto), akizungumza jambo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ofisi ya Mhe. Waziri, Jijini  Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kikao kati yao kilichofanyika jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Posted by MROKI On Friday, October 11, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo