Nafasi Ya Matangazo

September 06, 2024

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Beijing China.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla, amesema Wizara hiyo ipo tayari kushirikiana na wawekezaji mbalimbali wa katika ya Mawasiliano walioonesha nia ya kuwekeza nchini.

Amesema hayo tarehe 06 Septemba, 2024 jijini Beijing, nchini China mara baada ya kushiriki mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Wawekezaji na Viongozi wa Kampuni mbalimbali zilizopo nchini China ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Bw. Abdulla amesema Wizara iko tayari kushirikiana na wawekezaji hao na imekwishaandaa programu itakayojulikana kwa jina la “From the Peak of Mount Kilimanjaro to Space” itakayohusu uundaji na urushaji wa satelaiti itakayoanza mwaka huu.
Wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza kwa upande wa Sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni kutoka Kampuni tatu ambazo ni pamoja na China Academy of Space Corporation (CASC) inayojishughulisha na masuala ya uundaji na urushaji wa satelaiti.

Kampuni nyingine ni China Electronics Corporation iliyoonesha nia ya kuwekeza katika Ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vifaa vya TEHAMA pamoja na Kampuni ya Transsion Group.
Katika Mkutano huo, Rais Samia amekuwa na mazungumzo na Viongozi wa Kampuni za China Academy of Space Corporation (CASC), China Electronics Corporation, Transsion Group, Weihua Group, China Railway Construction Corporation (CRCC) pamoja na Acme Consultant Engineers PTE Limited na CND zote za China.
Posted by MROKI On Friday, September 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo