Nafasi Ya Matangazo

September 22, 2024




Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Yusuph Nzowa amehimiza washiriki wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa, (SHIMIWI) kudumisha upendo baina yao.

RAS Nzowa ametoa kauli hiyo leo alipoitembelea timu yake ya RAS Kilimanjaro,  ambayo inashiriki kwenye michezo hiyo kwa kushiriki kwenye michezo ya kuvutana kwa kamba, mpira wa miguu na netiboli.

Amesema michezo hii inadumisha ushirikiano, undugu na urafiki baina ya watumishi wa mahala fulani pa kazi na pengine.

“Hii michezo ni mizuri sana inaunganisha watu wa sehemu moja na nyingine na hata kusaidia mtu mmoja na mwingine, hivyo tudumishe upendo na kucheza kwa kupendana na kwa amani,”amesisitiza RAS Nzowa.

Hatahivyo, amewataka washiriki kuhakikisha wanawatumia watumishi halali ambao wapo kwenye utumishi wa umma na sio kutumia watu wan je ya utumishi wa umma kwani sio lengo la mashindano haya.
Katika hatua nyingine michezo ya netiboli iliyochezwa leo kwenye viwanja vya Jamhuri A na B, timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wamewafunga Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa magoli 44-8; huku RAS Dodoma wakiwachezesha kwata Wizara ya Mambo ya Ndani kwa maboli 27-4; nao RAS Singida waliwachapa Katiba na Sheria kwa magoli 24-17 na RAS Iringa waliwaliza RAS Kilimanjaro kwa magoli 42-0.

Michezo mingine ya netiboli Wizara ya Elimu waliwafunga Tume ya Khaki za Binadamu na Utawala Bora 41-6; huku RAS Mwanza wamewachapa Bodi ya Pamba kwa 27-2; nao Maendeleo ya Jamii waliwazamisha RAS Dar es Salaam kwa 28-13;Wizara ya Ujenzi waliwadadavua OSHA kwa 42-10; BRELA waliwachapa Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo kwa 21-19; nayo Wizara ya Afya ilitoa kipigo kwa Mashtaka kwa 44-16;RAS Singida wamewashinda Katiba na Sheria kwa 24-17; Wizara ya Maliasili na Utalii waliwafunga Wizara ya Nishati kwa 27-12;Ofisi ya Rais Ikulu waliwachapa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa 44-8; na Mahakama waliwachapa Wizara ya Mambo ya Nje kwa 35-25.
Katika mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Morgoro timu ya Wizara ya Uchukuzi waliwafunga Uwekezaji kwa magoli 8-0; huku kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mazimbu RAS Kilimanjaro waliwafunga Ofisi ya Wakili Mkuu kwa bao 1-0; huku Ofisi ya Mashtaka ya Taifa wametoka sare na Ulinzi kwa magoli 3-3; Maendeleo ya Jamii waliwaliza Wiara ya Kilimo kwa bao 1-0;Wizara ya Maji wamewafunga bila huruma Tume ya Utumishi wa Umma magoli 7-0.

Katika mechi nyingine za mpira wa miguu Wizara za Afya na Mambo ya Ndani wamesuluhu; huku Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wamewafunga RAS Simiyu kwa goli 1-0; Ofisi ya Mashtaka ya Taifa wamewachapa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera 2-0; Wizara ya Nishati wameshinda dhidi ya RAS Singida kwa 3-0; nao Wizara ya Ujenzi waliwafunga RAS Lindi kwa 1-0;wakati TARURA wameshinda dhidi ya Tume ya Maadili kwa Umma kwa 2-0; na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wamewashinda RAS Tanga kwa magoli 6-1.  

Katika mchezo wa kuvutana kwa kamba kwa wanawake timu ya Uwekezaji waliwavuta Wizara ya Mambo ya Ndani (1-0); Wizara ya Kilimo waliwavuta RAS Shinyanga (1-0); Hazina waliwavuta Wizara ya Mambo ya Nje (1-0);Tume ya Sheria waliwavuta Wizara ya Viwanda na Biashara (1-0); Ofisi ya Waziri Mkuu Sera waliwavuta RAS Singida (2-0);RAS Kilimanjaro waliwavuta Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (1-0); Ofisi ya Mashtaka ya Taifa wamewavuta Wizara ya Mifugo na Uvuvi (1-0); na Katiba na Sheria wamewavuta Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) (2-0).

Katika michezo mingine ya wanaume Mahakama wamewavuta Haki za Binadamu na Utawala Bora (2-0); Wizara ya Maji wamewavuta Ofisi ya Bunge (2-0); Wizara ya Ardhi wamewavuta Bodi ya Pamba (2-0);     
Posted by MROKI On Sunday, September 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo