Nafasi Ya Matangazo

September 29, 2024





Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wizara ya Mambo ya Ndani na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora zimetwaa ubingwa wa mchezo wa mbio za baiskeli kwa wanawake katika michuano ya michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa, inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali mkoani Morogoro.

 Mwanadada Alavuya Ntalima wa Mambo ya Ndani amemaliza mbio za Kilometa 30 kwa wanawake kwa kutumia saa 1: 39 zilizoanzia eneo la stendi ya Mafiga hadi Lugono na kurudi Stendi ya Mafiga; 

Ushindi wa pili kwa wanawake umetwaliwa na Scolastica Hasiri wa Wizara ya Uchukuzi kwa kumaliza kwa saa 1:40 na ushindi wa tatu umekwenda kwa Donansia Swai wa Hazina aliyetumia saa 1:47.

Kwa upande wa wanaume ubingwa umechukuliwa na mwendesha baiskeli mkongwe Hassan Ligoneno wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora baada ya kushinda kilimeta 50 zilizoanzia eneo la Stendi ya Mafiga kwa kutumia saa 2:07.

Ushindi wa pili kwa wanaume umechukuliwa na Chaacha Ikwabe wa Takukuru aliyetumia muda wa saa 2:08 na ubingwa wa tatu umekwenda kwa John Mgave wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa muda saa 2:10.

Michuano hii itaendelea kesho Jumatatu kwa mechi za hatua ya nusu fainali ya michezo ya riadha mita 100,200, 400, relay 4X100; 1,500, 800 (me) na mita 100 (me) za watumishi wenye umri umri mkubwa wa kuanzia miaka 50 na mchzo wa vishale (darts)
Posted by MROKI On Sunday, September 29, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo