Nafasi Ya Matangazo

August 05, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, ametembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kupata maelezo ya shughuli zinazofanyika pamoja na kupata maelezo kuhusu namna maonesho ya Nanenane kitaifa yanavyoendelea.

Mhe. Dendego ambaye mkoa wake pamoja na mkoa wa Dodoma ni wenyeji wa maonesho haya yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, amepewa maelezo na maafisa waandamizi wa DIB, Bw. Daudi Mwakalinga na Bw. Romuli Mtui.

Katika maelezo yao maafisa hao wameeleza kuridhishwa kwao na maandalizi ya maonesho haya licha ya changamoto ndogo za hapa na pale. Naye Mkuu wa Mkoa ameeleza matumaini yake kwamba maandalizi ya maonesho haya yatazidi kuwa bora jinsi miaka inavyokwenda. Mhe. Dendego aliambatana na baadhi ya viongozi walio katika kamati ya maandalizi ya maonesho hayo.

Posted by MROKI On Monday, August 05, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo