Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto) wakishuhudia makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana Kongwa kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Profesa Erick Komba (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS TRUST, Yohane Ibrahim Kaduma, Mei 13, 2024. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shamba la Mifugo Taliri Kongwa mkoani Dodoma. Kulia ni Balozi wa Denmark nchini, Matte Norgaard Dissing-Spandet. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 13, 2024 amezindua na kushuhudia makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana kilichopo Kongwa mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya makabidhiano ya kituo hicho, ambacho kinathamani ya shilingi bilioni 1.63 ikijumuisha uwekezaji wa vifaa na mindombinu, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza uwekezaji utunzwe ili taifa liweze kunufaika kupitia uwezeshwaji wa vijana.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwapatia vijana ujuzi kwa vitendo ikiwemo elimu ya ujenzi wa mabanda, ulishaji, matibabu na usimamizi wa mbuzi lakini pia kutoa mafunzo ya biashara ili vijana waweze kuwa wajasiriamali na kuendeleza biashara ya unenepeshaji mbuzi.
0 comments:
Post a Comment