Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia wakati akifungua Mkutano wa Viongozi wa
Kimataifa wa Taasisi ya Care International uliofanyika Hyatt Regency Jijini Dar
es salaam tarehe 13 Mei 2024.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDPn2jQXjlm2r5T65yubatrED-723MUGNc4nFVv2LKQz2A1utOyrzKWvJEWt7RJCYtwFtUl_QRy8UN91qNa3MCr_cXOUSDO0GpXPSRn6r8DzhuCBcn3WUGrJ7Mr0FHGbTbaNH1AvRjDlYIaD7SZCe48QqQH3Wu01_NcEW0d-48OfXjBas0exQM31qwcVM/w640-h420/D0004.jpg)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Care
International Marekani Bi. Michelle Nunn mara baada ya kufungua Mkutano wa
Taasisi hiyo uliyofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es salaam tarehe 13 Mei
2024. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Care Tanzania Bi. Prudence
Masako.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe pamoja
na Viongozi wa Taasisi ya Care International wakati alipowasili Hyatt Regency
Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi wa Taasisi hiyo
tarehe 13 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe pamoja
na Viongozi wa Taasisi ya Care International wakati alipowasili Hyatt Regency
Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi wa Taasisi hiyo
tarehe 13 Mei 2024.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizFEWGUpw_qFB-MXOhNYmezOv-epxAj1zi6KSN6EnE1dSlVO5HIiHd07KyYcK_YGgDCaOne6Zo370gGN64LI9wgZQ5hMtC5JnYUpxq3tirHCD2-gMOxgKoya4YNuDA7y5f8eX-q5SeWhVsAl-ZmBlUQZMOMy3qO-WbQUGBMlIpM9jRM0-FdL2Ji93s2LQ/w640-h406/D5.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe , Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Amani Mafuru katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Care Internation mara baada ya kufungua Mkutano wa Taasisi hiyo uliyofanyika Hyatt Regency Jijini Dar es salaam tarehe 13 Mei 2024.
************
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango ametoa wito kwa
Taasisi ya Care International kushirikiana na kuiunga mkono Tanzania katika
masuala ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo udhibiti na kukabiliana na maafa
pamoja na kujenga uwezo wa mfumo wa tahadhari za mapema.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua
Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa wa Taasisi ya Care International uliofanyika
Hyatt Regency Jijini Dar es salaam. Amesema ushirikiano unaweza kuongezwa zaidi
katika kujenga uwezo wa kustahimili mabadiliko ya tabianchi katika kuwezesha
kilimo cha kisasa kinachoendana na hali ya hewa ili kuboresha tija na mavuno
kwa wakulima wadogo.
Aidha Makamu wa Rais amewasisitiza viongozi wa Taasisi
hiyo kuunga mkono Tanzania katika programu mbalimbali za kuinua wanawake
kiuchumi ikiwemo matumizi ya nishati safi. Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari amezindua Mradi wa Nishati
Safi ya kupikia utakaowasaidia wanawake Barani Afrika (AWCCSP) pamoja na
Kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa nishati safi ya kupikia 2024-2034 ambapo
ushirikiano na wadau unahitajika ili kulinda mazingira na kuokoa Maisha ya
wanawake kutoka kutumia nishati isiyo rafiki hapa nchini.
Pia amewahimiza kuongeza ushirikiano katika
kuwawezesha ujuzi wavulana na wasichana walionje ya mfumo wa elimu kwa lengo la
kuwainua kimaisha na kuwajengea maendeleo mazuri ya baadae.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema ushirikiano
unahitajika katika tafiti na mipango ya
namna ya kupunguza changamoto ya afya ya mama na mtoto inayozikabili nchi za
kusini mwa jangwa la sahara. Ameongeza kwamba ni muhimu kufanyia tafiti suala
la kuongezeka kwa kuzaliwa watoto kabla ya wakati (njiti) pamoja na suala la
udumavu linaloikabili Tanzania licha ya kuwa nchi tegemeo kwa chakula.
Makamu wa Rais amesema kupitia juhudi za ushirikiano
kati ya Serikali, CARE International na washirika mbalimbali, mafanikio makubwa
yamepatikana kama ilivyoonyeshwa na viashirio muhimu vya maendeleo.
Amesema idadi ya watu wanaoishi chini ya
mstari wa umaskini wa mahitaji ya msingi imekuwa ikipungua kutoka 34.4% mwaka
2007 hadi 26.4% mwaka 2017-2018 na ilikadiriwa kuwa 25.7% mwaka 2020 . Ametaja
kupungua kwa kiwango cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano kutoka
vifo 81 hadi 43 kwa kila vizazi hai 1,000 kati ya 2010 na 2022. Idadi ya watu
wanaopata maji safi na salama iliongezeka kutoka 74.5% hadi 79.6% vijijini na
kutoka 86.5% hadi 90%. maeneo ya mijini, kati ya 2021 na Februari 2024. Kiwango
cha uandikishaji shule za msingi na Sekondari kilifikia 92.7% na 89.1% mwaka
2024 na usawa wa kijinsia wa 1:1. Amesema hadi kufikia Februari 2024, vijiji
11,837 kati ya vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara viliunganishiwa umeme,
sawa na asilimia 96.1.
Kwa
upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameipongeza Taasisi ya CARE Tanzania
kwa kujikita katika kuwasaidia wakulima kuwezesha kufanya kilimo bora na uchakataji
wa mazao hususani ya zao la chai. Amewapongeza kwa kuwezesha ujenzi wa kiwanda
cha mfano cha Uchakataji Chai cha Sakare kilichopo Korogwe mkoani Tanga na
kuwezesha masoko kupitia mtandao.
0 comments:
Post a Comment