Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali,
wadau wa Nishati pamoja na Washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya
UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024. Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa
Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha
ya pamoja na Wenyeviti Wenza, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre wa pili kutoka kulia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wa kwanza kulia pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA) Mhe. Dkt. Fatih Birol wakati
wa Mkutano wa Kimataifa wa
Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14
Mei, 2024.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Wenyeviti
Wenza, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre wa pili kutoka
kulia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wa
kwanza kulia wakati wa Mkutano wa
Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14
Mei, 2024.
Viongozi, Wadau wa Nishati pamoja na Washiriki
mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa
Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14
Mei, 2024
Viongozi, Wadau wa Nishati pamoja na Washiriki
mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa
Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14
Mei, 2024
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na
Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre kabla ya
kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa
wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14
Mei, 2024.
****************
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema licha ya Afrika
kuwa na idadi kubwa ya watu na raslimali zote muhimu, ni bara la chini kuwa na
upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.
Zaidi ya Waafrika milioni
900 wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia, jambo ambalo linachangia uharibifu
wa mazingira, upotevu wa bioanuai na athari za kiafya.
Rais Samia amesema nishati
safi ya kupikia ina maeneo matatu. La kwanza hasa maeneo ya vijijini ni uwezo
mdogo kutokana na gharama kubwa na upatikanaji wake pia ni tabu.
La pili ni ulimwengu kwa
jumla kutolipa suala hilo kipaumbele. Ufadhili mdogo na watu kutokujua fursa za
kiuchumi zilizopo kwenye nishati safi ya kupikia inayorejesha nyuma harakati
hizo.
Na pia kutokuwepo
ushirikiano wa kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa wote. Rais
Samia amesistiza upatikanaji, gharama ndogo na suluhu zinazotekelezeka.
Rais Samia pia amesema
kuongezeka kwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia itasaidia wanawake kupata
fursa zaidi kushiriki shughuli nyingine za kiuchumi, kupunguza umaskini na
usawa wa kijinsia.
Licha ya changamoto hizo,
Tanzania ina dhamira ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia
uliozinduliwa hivi karibuni uliokusudia kufikia 80% ya Watanzania wanaotumia
nishati hiyo ifikapo mwaka 2034.
Mkutano huu umehudhuriwa na
zaidi ya watu 1000 wakiwemo Marais, Viongozi mbalimbali, Asasi za Kiraia, Watu
mashuhuri wenye ushawishi kwenye masuala ya nishati safi na
wengine wengi.
Malengo hasa ni kuhakikisha
mbali na Afrika kupata uelewa lakini pia liwe jambo la Kimataifa ambapo pia
itakuwa rahisi kuchangia ili kuweza kutekeleza azma hiyo.
Pia nia ni kuandaa sera
madhubuti inayotekelezeka kwa ajili ya nishati safi ya kupikia na kuharakisha
ushirikiano wa wadau katika suala hilo.
Inakadiriwa kuwa dola za
kimarekani bilioni 4 zinahitajika kila mwaka ili kufanikisha upatikanaji wa
nishati safi ya kupikia kwa Waafrika wote ifikapo mwaka 2030.
Mkutano huu umeandaliwa
nchini Ufaransa na Shirika la Nishati Duniani (IEA) ambapo Rais Samia Suluhu
Hassan ndio Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika.
0 comments:
Post a Comment