Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza katika Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa, akitoa Neno la Utangulizi wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Baadhi ya washiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Baadhi ya washiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Muwakilishi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo nchini (IFAD) Bi. JacquiIine Machangu Motcho, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, akiweka mbegu ya Samaki katika moja ya Bwawa, wakati wa Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
Baadhi ya washiriki, baada ya Uzinduzi wa mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA), uliyopo chini ya Progamua ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), katika kijiji cha Mpitimbi Wilayani Songea Vijijini Tarehe 4 Mei, 2024
*************
Na Mwandishi Wetu – SongeaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe Jenista Mhagama amezindua Mradi wa kuendeleza lishe na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA) katika kijiji cha Mpitimbi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma Tarehe 4 Mei 2024.
Mradi huo wa kuendeleza lishe
na ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa wakulima wadogo (ARNSA) unaoenda
kutekelezwa katika Wilaya nne za Mikoa ya Ruvuma na Lindi, na kulenga katika
kunufaisha kaya elfu Moja (1000) katika Wilaya za Songea vijijini, Mbinga
Mkoani Ruvuma, Ruhangwa na Mtama Mkoani Lindi, ambapo pamoja na mambo mengine
Familia na jamii hizo zinaenda kuinua hali ya maisha kwa kuongeza kipato na
kuimalisha Lishe.
Akiongea katika uzinduzi wa
mradi huo,Waziri Mhagama alisema Mpitimbi imebahatika kuanza na mradi huu, na
kwakuwa Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula lakini, una
changamoto ya udumavu,”Na ndiyo maana Serikali imeleta mradi huu ambao utatumia
takribani zaidi ya shilingi Bilioni tatu nukta moja, katika maeneo
tuliyojipangia, ambao ni sehemu ndogo tuu ya Programu kubwa ya kuendeleza sekta
ya Kilimo na Uvuvi, Tumebahatika kuanza na mradi huu unaofadhiliwa na ubalozi
wa Norway Nchini hivyo ni wakati mzuri wa Wilaya zitakazonufaika kuweza
kujikimu kimapato na kiafya.” Alisema.
Aliendelea kusema kuwa, kwa
kuwa hali ya udumavu inaleta changamoto
ya afya ya akili ni fursa sasa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kuendelea
kuboresha afya, kupitia lishe ya viumbe maji na hasa Samaki.
Waziri Mhagama aliushukuru
ubalozi wa Norway kupitia shirika lake la NORAD kuleta mradi huo mkoani Ruvuma,
“Leo Tunazindua Shamba Darasa Ambalo linaenda kuchagiza maendeleo ya tabianzuri
ya biashara na matumizi ya lishebora kupitia samaki wanaofugwa kwenye mabwawa,
na miradi itakayofanywa kwenye baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Ruvuma.”
Alisisitiza.
Alibainisha kuwa, Kupitia
bwawa kubwa la Asili lililopo Mpitimbi ni wakati sahihi sasa wa kuimarishwa kwa
bwawa hilo na kuanza kwa ufugaji mkubwa wa Samaki “Tunatamani kuona kuwa Bwawa
hilo lenye ukubwa wa hekari 17.4 linaendelezwa na kuwa shamba Darasa.” Alisema
Awali, Waziri Mhagama
Alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa, kupeleka Miradi mingi ya Maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Naibu Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa
alisema, kupitia mradi huo unaoenda kutekelezwa kwa miaka miwili,Tanzania
imekuwa Miongoni mwa nchi tatu za Afrika kupata bahati ya kunufaika na Mradi
huo, zikiwemo nchi za Kenya na Msumbiji.
Aliendelea kusema kuwa, mradi
huo wa kuendeleza Lishe na ufugaji
endelevu wa viumbemaji na ukulima wa mwani
kwa wakulima wadogo unatekelezwa katika mikoa kumi na moja ya Tanzani
Bara pamoja visiwa vya unguja na Pemba.
Akiongea katika ghafla hiyo muwakilishi kutoka Mfuko wa
Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo nchini (IFAD) Bi. JacquiIine Machangu Motcho aamesema, IFAD imekuwa
ikifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania katika nyanja na sekta zinazolenga, kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikumba sekta ya kilimo hususani Wakulima wadogo wadogo hasa wale walio
vijijini.
Na aliendelea kusema kuwa, Shirika hilo
limeendelea pia kuyapa kipaumbele maeneo
hayo ikiwa na dhamira ya kuinua na kuboresha sekta ya Kilimo, Mazao, Mifugo na
Uvuvi ili kufikia uzalishaji wa juu ulio endelevu na wenye faida kibishara,
unaoleta ukuaji wa pamoja kiuchumi na Taifa zima kwa ujumla.
Akizungumza kuhusu mradi huo, Bi JacquiIine alisema Kupitia Programu ya
kuendeleza Kilimo na Uvuvi, IFAD imepokea ufadhili-ruzuku(grant) kwa mradi wa
ARNSA kutoka Ubalozi wa Norway, unaolenga kupunguza umaskini na kuboresha lishe
kupitia shughuli za Ufugaji wa Samaki wenye tija na ustahimilivu kutoka kwa
wazalishaji/wafugaji wadogo. Dhamira yake ya kimaendeleo inalenga kuongeza
mapato, kujenga ustahimilivu na kuwajengea uwezo kimaisha wafugaji wadogo wa
samaki walio vijijini.
0 comments:
Post a Comment