Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu(katikati) akitoka kukagua utengenezaji wa milango inayowekwa kwenye jengo la Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba,wengine ni wahandisi wa mradi na viongozi wa idara na vitengo alioongozana wakati wa ukaguzi uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa(NHC),Peter Mwaisabula akitoa maelezo ya lifti kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ally Senga Gugu(wanne kushoto) wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba,wengine ni wahandisi wa mradi na viongozi wa idara na vitengo walioongozana na Katibu Mkuu wakati wa ukaguzi uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu(aliyenyoosha mkono)akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa(NHC),Peter Mwaisabula alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba,wengine ni wahandisi wa mradi na viongozi wa idara na vitengo alioongozana wakati wa ukaguzi uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
**************
Na Mwandishi Wetu,DODOMAKatibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu amemtaka mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa
Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba kuwasilisha
mpango kazi wa mradi huo baada ya kuwepo kwa ucheleweshaji wa umalizaji wa
mradi huo ambapo hapo awali ulipaswa kumalizika oktoba mwaka jana na kuongezewa
muda wa makabidhiano kuwa mwezi huu mwishoni lakini hadi sasa hakuna dalili za
kukabidhiwa mradi huo kwa muda ambao mkandarasi aliomba kuongezewa.
Akizungumza baada ya ukaguzi
wa mradi wa ujenzi huo,Katibu Mkuu Ally Senga Gugu amesema mapokeo ya fedha za
mradi kutoka Wizara ya Fedha yamekua mazuri lakini kwanini kumekuwepo kusuasua
kwa mradi huo huku akimtaka Meneja Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania(TBA)
kuwasiliana na kumsimamia mkandarasi ambae ni Shirika la Nyumba la Taifa ili
aweze kumaliza mradi huo ili wizara waweze kukabidhiwa jengo likiwa
limekamilika.
‘Hii ni taswira labda
anaetenda kazi na anaesimamia kazi mawasiliano hayapo vizuri,aidha hamsikilizi
au aambiwi kwasababu msimamizi anasema anatoa maelezo kwa kila namna lakini
mtendaji anaongea lugha tofauti,inakuaje kifaa kikubwa kama lifti kinakuja
kinafungwa bila kuwepo usimamizi wowote na hakuna zuio lolote,leo tunatakiwa
tupandishwe lifti hii ni kama kitu kilifungwa usiku alafu asubuhi mkashtukia
kimefungwa,kwahiyo bado aitupi taswira nzuri ya eneo lenu la kazi jinsi
mnavyosimamiana kazi sasa tutoe maelekezo hilo lifanyiwe kazi ipasavyo,na kuna
mambo yapo kwenye ngazi ya wizara tutaongea na sekta nyingine ili kuhakikisha
mradi wetu unatimia nachowaomba wasilisheni mpango kazi ili tuone mtamalizaje
ndani ya wakati uliobakia ambao ni muda mfupi sana bado siku kumi tu’ alisema
Katibu Mkuu Ally Senga Gugu
Akizungumza mbele ya Katibu
Mkuu wakati wa ziara hiyo,Mhandisi wa Mradi kutoka Shirika la Nyumba la
Taifa(NHC),Peter Mwaisabula amesema ni kweli awakamilisha asilimia mia ya kazi
za nje kama sasa hivi kazi ya ujenzi wa uzio bado imesimama kwa sababu chuma
zilichelewa kufika na kuhusu kuweka vitofali tumebakiza sehemu ndogo na tuna
hakika kufikia mwisho wa mwezi zile kazi za msingi tutakua tumezimaliza na
tumechukua maelekezo yako kiongozi na
tutayafanyia kazi.
Naye Msimamizi wa Mradi
anaetokea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Iddy Msangi alisema maelekezo ya
serikali kutoka ofisi ya Waziri Mkuu na kutotoa kipaumbele cha kuongezewa muda
kwa mkandarasi anaeshindwa kumaliza kazi zake kwa wakati huku akielezea mud awa
kuisha mradi na jinsi mkandarasi anavyosuasua kumaliza mradi kwa wakati.
Mradi huo wa Ujenzi wa Ghorofa
Tano ni moja ya miradi ya Maofisi ya Wizara yanayojengwa katika Mji wa Serikali
Mtumba,jijini Dodoma na Katibu Mkuu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Munngano wa
Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani amekua akiipatia wizara hela ya
kugharamia mradi huo kila wizara inapoomba fungu hilo.
0 comments:
Post a Comment