Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa (wa pili kushoto) akikabidhi taulo za kike kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwananyamala B,Modeta Mushi, zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwasitiri watoto wa kike.Wengine pichani ni Afisa Mawasiliano wa Barrick, Neema Ndossi na Mkaguzi wa Polisi Kitengo cha Usalama barabarani Amina Said.
Na Mwandishi Wetu.
Katika dhamira yake ya kuhakikisha Watoto wa kike na wanawake wanapata elimu kuhusu umuhimu wa usafi katika kipindi vya hedhi, Barrick Tanzania imeshiriki maadhimisho ya siku hii ambayo⁹ huadhimishwa Mei 28 kila mwaka ambapo wafanyakazi wake walishiriki kugawa taulo za kike kwenye makundi mbalimbali yenye mahitaji ikiwemo kwa wanafunzi wa shule ya msingi zilizopo jirani na maeneo ya migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na ofisi ya Dar es Salaam.Vile vile imeshirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama barabarani kutoa elimu ya usalama kwa Wanafunzi.
Wanawake wengi na wasichana katika jamii zetu hupata changamoto kubwa katika kipindi cha mzunguko wao wa mwezi wa siku za hedhi, kutokana na kutoweza kumudu kununua pedi za kutumia,ukosefu wa elimu kuhusiana na hali hiyo.imani za mila ambazo zinawafanya wengi kuamini kuwa suala la hedhi halipaswi kuongelewa,ukosefu wa mazingira rafiki ya kujihifadhi mtu anapokuwa kwenye hali hiyo kama vile vyoo na maji safi ya kutumia. Changamoto hizo zote zinasababisha watumie vifaa vya kuwasitiri visivyofaa ambavyo vinaweza kuwasababishia kupata maradhi.
Wanafunzi wakipatiwa mafunza ya usafi katika hedhi na usalama kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick na Jeshi la Polisi
---
Barrick inaamini Siku ya Usafi wa Hedhi Salama Duniani ni maalumu kwa ajili ya kuvunja ukimya na kujenga ufahamu kuhusu umuhimu mkubwa wa kutunza usafi wakati wa hedhi. Siku hii inaangazia changamoto mbalimbali ambazo wanawake na wasichana kote duniani wanakabiliana nazo kuhusiana na hedhi, ambazo zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa afya zao, elimu yao na hali yao ya maisha kwa ujumla.
Kwa kuunga mkono siku hii muhimu, Barrick inachangia katika kujenga jamii yenye usawa, afya, na ufahamu zaidi, ambapo kila mwanamke na msichana anaweza kujitunza kwa ujasiri na heshima wakati wa hedhi yake.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwananyamala B wakifurahia zawadi za taulo za kike walizopewa kwa ajili ya kuwasitiri.
0 comments:
Post a Comment