Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto)
akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi wa Ofisi hiyo, Bi. Philomena Malembo
mara baada ya kuwasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo
Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam Aprili 4, 2024 kwa ajili ya kujitambulisha
kwa Viongozi na Watendaji kufuatia uhamisho wake kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi hiyo, Bw. Elisha Msengi mara baada ya kuwasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam Aprili 4, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian
Luhemeja (kulia) kwa ajili ya kumkaribisha Mhandisi Luhemeja mara baada ya
kuwasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Mtaa wa Luthuli
Jijini Dar es Salaam Aprili 4, 2024 na kujitambulisha kwa Viongozi na Watendaji
kufuatia uhamisho wake kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu). Katikati ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5hvFbN-MyuZ5yKKHPcDKbGNbMCW2uQIurZGC9OPDujKktMbgnoPRqamiRMLGCs-gm8BPH2JyL0xTwA18LLItvobyfKxFU3vOQhey76lg8PjH2ozQUu0tYXj1BUXDRAKXfq-TL_7BUGdKeg7guExVqQFqlfwR7JtLH4boG_gxo3kauYeEEHb-TNgnWfMo/w640-h294/8.JPG)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na
Watendaji wa Ofisi hiyo wakati wa utambulisho wa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo,
Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw.
Abdallah Hassan Mitawi (kulia) wakati wa kumkaribisha Mhandisi Luhemeja mara
baada ya kuwasili katika ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo Mtaa
wa Luthuli Jijini Dar es Salaam Aprili 4, 2024 kwa ajili ya kujitambulisha kwa
Viongozi na Watendaji kufuatia uhamisho wake kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi
hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia kwa Waziri Jafo) pamoja na Watendaji
Waandamizi wa Ofisi hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa shughuli ya utambulisho
wa Mhandisi Luhemeja katika Ofisi ndogo za Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo
Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam Aprili 4, 2024.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpEAAxYujBSgIFYxK2gZCrDorX0rKMozzXVEL2CObXS0gAp-rIu8qvPpVfMrVK0tq-vO7Der3SrJKyZYyhnyPGd4oDCLpCtCuFVJFP3AhDKobAntUEiNrl_LduVRpHk7Z-ER0mmlUebpDD4ApEpLgh1lmZXhpx5Ev52Rm49YpzhsQPtByat_Lipja8MM8/w640-h486/11.JPG)
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian
Luhemeja akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah
Hassan Mitawi (katikati) na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme
(kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi ndogo za ofisi ya zilizopo Mtaa wa
Luthuli Jijini Dar es Salaam Aprili 4, 2024 ***********
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa
maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja kuimarisha
kasi ya usimamizi wa biashara ya kaboni, ajenda ya nishati safi ya kupikia na
utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Sura 191 ili kuhakikisha sekta ya mazingira
inaleta tija kwa Watanzania.
Dkt. Jafo amesema
hayo Aprili 4, 2024 wakati wa utambulisho wa Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi hiyo,
Mhandisi Cyprian Luhemeja aliyehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka Ofisi
ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu).
Mhe. Jafo amesema
majukumu ya Ofisi hiyo yamezidi kufahamika kwa haraka zaidi na Watanzania
kutokana na manufaa yake kugusa maslahi moja kwa moja ya jamii huku akitolea
mfano ajenda ya nishati safi ya kupikia na kueleza kuwa Serikali imepanga kuja
na mkakati mahsusi wa kuwakomboa wanawake katika kuachana na nishati chafu ya
kupikia.
Akifafanua zaidi
Dkt. Jafo ameeleza kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa nishati safi ya kupikia kwa
wanawake wa Kitanzania, Serikali imeweza mazingira wezeshi ya kuhakikisha
upatikanaji wa nishati hiyo ikiwemo kupunguza gharama ya ununuzi wa vifaa na
tayari wadau wengi wameonesha dhamira ya kuunga mkono juhudi hizo.
“Mnakumbuka kuwa
Ofisi yetu imepewa maelekezo na Mhe. Rais ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati
safi ya kupikia kwa wanawake ifikapo mwaka 2030…Hivyo hatuna budi kuandaa
mkakati mahsusi wa kuhakikisha kuwa dhamira hiyo inafikiwa na kutekelezeka”
amesema Dkt. Jafo.
Aidha Dkt. Jafo
amesema mwezi Mei mwaka huu kutafanyika Mkutano mkubwa utakaojadili ajenda ya
nishati safi ya kupikia nchini Ufaransa na kupitia mkutano huo Serikali ya
Tanzania imejipanga kutumia fursa hiyo kuonesha jitihada mahsusi ilizochukua
katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake.
Akizungumzia
Biashara ya Kaboni, Dkt. Jafo amesema Serikali imeandaa kanuni na mwongozo wa
biashara hiyo kupitia usimamizi wa Kituo cha Kitaifa cha Uratibu wa Kaboni
(NCMC) kilichopo Mkoani Morogoro ambapo wawekezaji mbalimbali wamejitokeza kwa
ajili ya uwekezaji na hivyo mkakati uliopo kuhakikisha jamii inajitokeza na
kushiriki katika biashara ili kujiongezea kipato.
Ameongeza kuwa
katika kujenga hamasa kwa jamii kushiriki katika biashara ya kaboni, Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imepanga kuendesha makongamano na mijadala
mbalimbali itakayoshirikisha Viongozi Wakuu wa Serikali pamoja na wadau wa
sekta ya mazingira na kuandaa mpango mkakati wa pamoja utakaoinisha fursa na
manufaa ya biashara hiyo kwa Watanzania.
Kwa mujibu wa
Waziri Jafo amesema hadi sasa jumla ya kampuni 42 tayari zimesajili miradi ya
biashara ya kaboni katika kituo cha NCMC na kuongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa
Rais imejipanga kuhakikisha makampuni mengi zaidi yanajitokeza kusajili miradi
yao sambamba na kuhimiza ushirikiano wa karibu na wadau wa biashara ya kaboni.
Kuhusu
utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191, Waziri Jafo amesema
Serikali imeanza kufanya marekebisho ya kubadili muundo wa Baraza la Taifa na
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa
Mazingira (NEMA).
Amesema kuwa
Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuwa hadi kufikia Juni 2024, Muswada wa
Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191 itawasilishwa katika
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zaidi.
“Marekebisho hayo
yatahusisha kubadili muundo wa NEMC ili kuwa Mamlaka na hatua hiyo itaweizesha
kutekeleza majukumu yake kwa nguvu zaidi na hivyo kuleta tija iliyokusudiwa
katika suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini” amesema Dkt. Jafo.
Kuhusu masuala ya
Muungano, Dkt. Jafo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kuratibu na
kusimamia vyema utatuzi wa hoja ambapo katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia
mwaka 2021 hadi 2024 jumla ya hoja 15 zimepatiwa ufumbuzi kupitia vikao vya
kamati ya pamoja baina ya SJMT na SMZ.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja amemshukuru
Waziri Jafo kwa maelekezo aliyotoa na kuahidi kusimamia utekelezaji wake kwa
kushirikiana na watendaji wengine wa ofisi hiyo ili kufikia dhamira na malengo
yaliyopo katika kuwahudumia
wananchi.
Kikao hicho
kilihudhuria pia na Watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi, Naibu Katibu Mkuu
(Mazingira) Bi. Christina Mndeme, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu,
Bw. Elisha Msengi, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware.
0 comments:
Post a Comment