Nafasi Ya Matangazo

April 06, 2024





Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji kwenye kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga Vijijini na kutaka bei mpya ziwe sawa na zile za Shinyanga Mjini mara moja.

Akiwa katika Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi, DC Mtatiro ameelekeza kuanzia tarehe 04.04.2024 bei za maji zishuke.

Mwakilishi wa Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amekiri kupokea maelekezo hayo kwenye mkutano huo na kuanza kuyatekeleza mara moja. 

Kuanzia sasa Bei za Maji kata za Didia, Tinde na Iselamagazi zenye jumla ya wakazi takribani 55,000 itakuwa shilingi 1,490 kwa wanaotumia uniti 1 - 5 kwa mwezi na shilingi 1,700+ kwa wanaotumia uniti 6+. 

Wananchi wa kata hizi kwa miaka mitatu mfululizo wamekuwa wakilipa bili za maji kwa uniti moja shilingi 2,525 na hakukuwa na suluhu kwa sababu SHUWASA na EWURA walikuwa wanavutana katika kufanya uamuzi husika. 

Katika mkutano huo, DC Mtatiro amekiri kumpigia simu Waziri wa Maji Juma Awesso ambaye ameunga mkono mapendekezo ya Wakili Mtatiro.

DC Mtatiro anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa zote 6 za Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni wilaya yake ya pili kuwa Mkuu wa Wilaya tangu Rais Samia amhamishe kutoka Tunduru Mkoani Ruvuma.
Posted by MROKI On Saturday, April 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo