Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa kupitia SUMAJKT kutokana na kazi kubwa wanayoifanya katika ujenzi wa nyumba 5000 uliogawanyika maeneo matatu tofauti Wilayani Handeni msomera na kilindi saunyi mkoani Tanga pamoja na simanjiro kitwayi B
Akizungumza Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka hiyo mara baada y kumaliza ziara yao ya kikazi katika kijiji cha Msomera, Jenerali (Mstaafu) Venance Mabeyo amesema kazi kubwa inayofanywa na jeshi katika ujenzi huo ni lazima iungwe mkono na wadau wengine wa kisekta ili kukamilisha zoezi hilo haraka.
Amesema katika ziara hiyo amejionea kusuasua kwa baadhi ya sekta katika utekelezaji wa majukumu yao hivyo kushauri kila mdau ni muhimu kuhakikisha anatekeleza majukumu yake.
“SumaJkt mnafanya kazi kubwa ni muhimu sana kila mmoja wetu atimize wajibu wake ili tuimarishe miundo mbinu ya kijiji hiki hasa nyumba ili wananchi waweze kuhamia kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro,”alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Kamishina wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Richard Kiiza amesema hamasa ya wananchi kuhamia katika kijiji hicho ni kubwa ambapo mamlaka itaendelea kuwahamisha kadri wanavyojiandikisha
Kaimu Operesheni Kamanda wa mradi huo Luteni kanali Edward Mwanga aliwahakikishia wakurugenzi hao wa bodi kuwa ujenzi wa nyumba hizo utakamilika kutokana na kasi na ari ambayo wanayo katika utekelezaji.
0 comments:
Post a Comment