Na Asila Twaha, OR - TAMISEMI
Mwenyekiti wa Waganga Wafawidhi Dkt. Florance Hilari amesema, hakuna sababu ya kutokufanya kazi sababu Serikali imeonesha dhamira njema kwa wananchi wake kuendelea kuboresha sekta ya afya nchini.
Dkt. Hilari ameyasema hayo tarehe 14 Februari, 2024 mkoani Dodoma wakati akisoma risala kwa niaba ya Waganga Wafawidhi wakati wa kufunga mkutano wa kwanza uliowakutanisha Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya ya msingi.
“Tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya katika kuboresha sekta ya afya nchini, sisi kama watendaji wake tumeona dhamira yake kwa wananchi” amesema Dkt. Florance
Amesema wao kama waganga wafawidhi hawana sababu ya kutofanya kazi huku ukizingatia zaidi ya asilimia 80% ya wananchi wote wanapata huduma ya afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi ngazi ya Halmashauri amesema, hivyo kwa jitihada Serikali wanazozifanya ni lazima ziambatane na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ambao sisi ndio tunapaswa kuitoa kwa wananchi.
Ameongeza kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo ya Wizara zinazosamia sekta ya Afya , Uongozi wa Mikoa huku tukijikita kwenye nguzo sita za Shirika la Afya na ile moja ya nchini kwetu ambayo ni usimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya.
Akiwasilisha changamoto za waganga wafawidhi Dkt. Hilary amesema wafawidhi wanafanya kazi kubwa sana kwenye vituo vya kutolea huduma ngazi ya msingi lakini hawana posho ya madaraka kitu kinachoshusha morali ya kazi na ikizingatia katika baadhi ya vituo Mfawidhi anakua peke yake hivyo anafanya kazi za utawala na kidakitari.
Pia aliiomba Serikali kuangalia namna ya kutoa mafunzo na ufadhili katika maeneo yatakayokuza kada hiyo huku wakiiomba Serikali kuona namna ya kufanya mapitio ya viwango vya posho ya kuitwa kazini "Oncall allowance”
Kwa upande wa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye ni mgeni rasmi katika kufunga kikao hicho akitolea ufafanuzi wa hoja zililotolewa na wataalamu hao huku akiahidi kuzifanyia kazi amesema, Serikali inathamini na kutambua majukumu yao na chini ya usimamizi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan atahakikisha kuanzia Julai, 2024 Waganga Wafawidhi hao wanaanza kulipwa posho.
Mkutano huo wa siku mbili uliowashirikisha Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya vya Serikali pamoja na Hosptitali za Kidini zenye makubaliano na Serikali ulifunguliwa na Mhe. Dkt. Festo Dugange Naibu Waziri wa TAMISEMI.
0 comments:
Post a Comment