Nafasi Ya Matangazo

February 13, 2024


Na Mwandishi wetu, Tunduru - Ruvuma
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro ametangaza kufungwa kwa barabara ya  Mangaka - Tunduru Mjini kufuatia kujaa maji kwa mto Muhuwesi ulioyopo wilayani humo mkoani Ruvuma.
 
Mtaturu amesema mvua kubwa zinazonyesha katika maeneo ya ukanda wa Morogoro na Selous, daraja kubwa la Mto Muhuwesi lililoko Tunduru limejaa maji hadi juu ya daraja na kwa hiyo tumechukua uamuzi wa haraka wa kufunga barabara kuu ya Mangaka - Tunduru Mjini kwa muda.
 
“Kutokana na mvua kubwa zinazonyesha ukanda wa Morogoro na Selous, daraja kubwa la Mto Muhuwesi lililoko Tunduru limejaa maji hadi juu ya daraja na kwa hiyo tumechukua uamuzi wa haraka wa kufunga barabara kuu ya Mangaka - Tunduru Mjini kwa muda. Eneo la barabara linalofungwa ni eneo la mto lililo kati ya Kata za Muhuwesi na Majimaji,” amesema Mtaturu.
 
Amesema magari yanayotokea Mbeya, Iringa, Songea na Mkoa wote wa Ruvuma kuelekea Mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam yanapovuka Tunduru  Mjini yapaki na kupumzika kusubiri hali iwe sawa Mto Muhuwesi.
 
Aidha, magari hayo yanaweza pia kusimama/kupaki na kusubiria Sisi kwa Sisi au Muhuwesi Kijijini.
 
Mtaturu amesema magari yanayotokea mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar Es Salaam kuja Tunduru, yanashauriwa kusimama na kupaki Nakapanya, Namiungo au Majimaji.
 
Madereva wasilazimishe kuvuka daraja hili kwa sababu wataleta madhara, lakini vyombo vyetu vya usalama vimechukua tahadhari zote, visikilizwe.

Posted by MROKI On Tuesday, February 13, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo