Nafasi Ya Matangazo

February 22, 2024

  WhatsApp%20Image%202024-02-22%20at%202.44.52%20PM
Na Mwandishi wetu, Morogoro
SHULE ya Msingi Mgulu wa Ndege Manispaa ya Morogoro yenye wanafunzi zaidi ya 1000 inakabiliwa na changamoto ya Matundu ya Vyoo vya walimu na wanafunzi.

Hayo yamebainika kwenye ziara ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz M. Abood alipofika shuleni hapo kukagua miradi ya maendeleo ya shule huyo.

Kufuatia changamoto hiyo Abood amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi Huku akichangia million moja katika ujenzi wa vyoo vya walimu na kumlipa fundi ili anze mara moja ujenzi huo.

Akiwa Shule ya Sekondari Mkundi Abood amejionea miundombinu na usomaji wa Wanafunzi na kuahidi kutoa Kompyta 7 kwa wanafunzi na Kompyuta mpakato 2 kwa walimu kwa lengo la kunoresha elimu.

Pia katika ziara hiyo Mbunge alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa kata ya Mkundi Ambao walikuwa na kero mbalimbali zikiwemo za maji,umeme na ubovu wa miundombinu ya Barbara.

Kupitia changamoto ya maji Abood alizungumza na viongozi wa idara ya maji Ambao waliahidi mbele ya wananchi kuwa baada ya wiki moja changamoto hiyo itapatiwa ufumbuzi.

Aidha Mbunge huyo amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Morogoro Mjini na kuwaelekeza wahusika kutunza Miradi hiyo.
Posted by MROKI On Thursday, February 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo